Mabao ya Messi yaficha aibu LaLiga

Muktasari:
- Idadi ya mabao aliyofunga nyota huyo wa Barca yanalingana na yaliyofungwa na nyota saba
Madrid, Hispania. LaLiga inashudia ukame mkubwa wa mabao jambo linalotia shaka, lakini ni mchezaji moja tu aliyefanikiwa kuficha aibu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu: Lionel Messi.
Ukiangalia vinara wa ufungaji katika kuwania tuzo ya Pichichi baada ya mechi 11, ni nyota wa Barcelona pekee aliyefunga mabao 12, baada ya Messi anayemfuata ni Simone Zaza aliyefunga mabao tisa na Cedric Bakambu amefunga saba, huku Rodrigo Moreno na Antonio Sanabria kila moja amefunga mabao saba.
Wachezaji hao wote ni wazuri katika klabu zao ndogo, lakini si washambuliaji wa nyota wanaotambulika duniani.
Wakati washambuliaji hao wakitamba, nyota waliozoelekeka katika orodha ya wafungaji wapo chini kwa sasa.
Katika orodha ya wafungaji waliofunga bao moja LaLiga inaongozwa na Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Kevin Gameiro huku Antoine Griezmann, Gareth Bale na Wissam Ben Yedder wakiwa wamefunga mabao mawili wakati Luis Suarez akiwa juu yao kwa kufunga mabao matatu.
Hivyo kuwafanya washambuliaji hao nyota saba kuwa wamefunga jumla ya mabao 12, ikiwa sawa na idadi ya magoli aliyofunga Messi peke yake.
Baadhi ya majina hayo yamepata anguko kubwa zaidi kulinganisha na msimu uliopita, akiwamo Ronaldo ambaye alikuwa amefunga mabao matano katika mechi nane za mwanzo wa msimu 2016/17, kuwa chini ya hapo ni jambo la kushangaza.
Benzema pia ameshindwa kufikia rekodi yake ya msimu uliopita, ya kufunga mabao matatu wakati kama huu, huku Griezmann akiwa katika wakati mgumu zaidi.
Pengo kubwa la kushuka kwa ufungaji lipo Camp Nou wakati Suarez amefunga mabaoa matatu akiwa nyuma kwa magoli matano aliyofunga baada ya mechi 11 msimu 2016/17.