Kutana na Jacob: Mtanzania mwenye bahati zaidi nchini

Meneja Uendeshaji wa Premier Bet, Samir Matar (kulia), Mshindi wa Mchezo wa Navigator Jacob Mkungilwa (katikati) na Meneja Rasilimali Watu wa Premier Bet, Amanda Kusila (kushoto) katika picha ya pamoja baada ya kumkabidhi mshindi huyo fedha taslimu Sh118 milioni.
Ushindi wa aina yoyote unaleta furaha lakini ushindi wa mamilioni ya fedha kupitia michezo ya kubashiri ya Premier Bet unakufanya uhisi dunia hii yote ni yako.
Premier Bet ni magwiji wa kuzalisha mamilionea kila uchwao na mwezi huu wa Julai, Jacob Mkingilwa ambaye ndiye mshindi wa mwezi Juni pia, ameibuka kinara kwa mara nyingine akiondoka na Sh118 milioni.
Michezo ya ubashiri ilionekana kama ni bahati ya mara moja tu mpaka pale Mkingilwa alipotudhihirishia kuwa ushindi kwake ni tabia.
Meneja Uendeshaji wa PremierBet nchini, Sami Matar akizungumza katika hafla ya kumtangaza mshindi wa mwezi Juni, alisema kuwa anajiskia fahari kumtangaza Jacob Mkingilwa mshindi kwa mara nyingine tena.
“Hii si mara ya kwanza kukutana na Bwana Jacob. Ninaweza kutangaza kwa kujiamini kwamba katika miezi ya Juni na Julai, Jacob amekuwa “kijana mwenye bahati zaidi nchini Tanzania.”
Juni 25 Bwana Jacob alishinda kiasi kikubwa cha Sh112 milioni, nadhani mnakumbuka mkutano wa waandishi wa habari tulioandaa kwa ajili yake karibu wiki mbili zilizopita.
Leo tunafurahi kuona kwamba ameshinda tena! Jacob alipokuwa akicheza mchezo wetu wa kusisimua wa kasino mtandaoni "Navigator" alipata bahati ya kushinda kiasi kingine kikubwa baada ya siku 17 tu tangu ushindi wake wa awali. Leo ameshinda Sh118 milioni hivyo kwa ujumla katika kipindi cha chini ya siku 30 ameshinda kiasi cha Sh230 milioni.

Meneja Uendeshaji wa Premier Bet, Samir Matar (kulia) akimkabidhi mfano wa Hundi ya Pesa Taslim Sh118 milioni Mshindi wa mchezo wa Navigator Jacob Mkungilwa (katikati) Kushoto ni Meneja Rasilimali Watu wa Premier Bet, Amanda Kusila katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kumkabidhi mshindi huyo.
Premier Bet, tunapenda kusisitiza ubashiri wa kistaarabu. Tunajitahidi kutoa jukwaa bora la michezo ya kuba-hatisha mtandaoni ambalo litampatia mchezaji furaha na burudani, huku tukiwahakikishia mazingira salama.
Kubashiri ni kwa watu walio na umri wa miaka 18 na zaidi pekee. Tunasi¬mamia sera ya Kubashiri Kistaarabu, tunataka wateja wetu kufurahia michezo yetu, na hivyo tunashauri wachezaji wasicheze zaidi ya uwezo wao kifedha.
Zaidi ya hayo, nafurahi binafsi kupata fursa ya kumshauri Jacob jinsi ya kuwekeza ushindi wake mpya katika kilimo na ujenzi wa nyumba nzuri kwa familia yake. Tunatumai atatumia ushindi wake kwa busara; Sh230 milioni bila shaka ni kiasi cha kubadili maisha. Hongera Jacob kwa bahati yako!
Amanda Kusila, Meneja wa Rasilimali Watu wa Premier Bet Tanzania, pia alisema yafuatayo: "Habari zenu ndugu waandishi wa habari, wateja wote wa Premier Bet na watanzania wenzangu. Napenda kumpongeza kwa dhati mshindi wetu wa Nguli, Bwana Jacob Mkungilwa kutoka Njombe, Tanzania.
Bwana Jacob ameshinda Sh118 milioni na tunafuraha kubwa sana kwani hii ni mara ya pili kwake kushinda kiasi kikubwa cha pesa, kama tunavyokumbuka wiki mbili zilizopita, tulikuwa hapa kusherehekea ushindi wake wa mkubwa wa Sh112 milioni. Nise-me tu Bwana Jacob, wewe ni mtu mwenye bahati sana, Hongera sana.”
Premier Bet ni kampuni ya kubashiri inayofanya kazi mtandaoni na nje ya mtandao, maana tuna mawakala na maduka. Na tukiwa hapa leo, ningependa kusisitiza umuhimu wa Kubashiri Kistaarabu, cheza kama burudani na usitumie pesa zote kwenye kubashiri.
Ofisa wa GBT, Jehudi Ngollo, alisema kuwa, “Kwa niaba ya Mkurugenzi wetu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, ningependa kumpongeza Bwana Jacob Mkungilwa kutoka
Njombe, Tanzania kwa ushindi huu usio wa kawaida. Na pia, kuwakumbusha wote kwamba kubashiri ni kwa ajili ya furaha na sio mbadala wa ajira. Ninaamini Kampuni ya Premier Bet na Benki wataendelea kumshauri mshindi wetu mwenye bahati Bwana Jacob jinsi ya kutumia kiasi alichoshinda kuwekeza na kubadili maisha yake.

Mshindi wa mchezo wa Navigator kutoka kampuni ya Premier Bet Jacob Mkungilwa akiwa tayari ameshapokea kiasi cha Sh Sh118 milioni.
Pia, ningependa kuwakaribisha nyote kwenye Banda la Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, Maonyesho ya Saba Saba, ambapo tunatoa elimu na kuhakikisha kila mtu anapata elimu kuhusiana na Kubashiri Kistaarabu.”
Kwa upande wake, Jacob Mkungilwa, Kijana Mwenye Bahati Zaidi nchini Tanzania, baada ya kutangazwa mshindi wa mwezi Julai, alisema kuwa, “Nina shukuru sana kwa fursa hii na bahati kubwa niliyopata. Premier Bet imenipa namna ya kipekee ya kufurahia mchezo wangu pendwa, Navigator, na siku¬fikiria kamwe kwamba ningeshinda si mara moja tu, bali mara mbili ndani ya mwezi. Ni ndoto ambayo imetimia.
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Kampuni ya Premier Bet kwa namna ya kipekee na ya kusisimua wanavyotoa michezo. Mchezo wa Navigator unavutia sana, na unaleta msisimko usio na kifani. Naishukuru sana timu ya Premier Bet kwa juhudi na kazi kubwa wanayoifanya ya kuunda mazingira ya kucheza michezo inayoleta furaha na yenye malipo.
Kwa utajiri huu mpya nilioupata, nimeazimia kufanya maamuzi mazuri na kuhakikisha natengeneza maisha mazuri kwangu na kwa wapendwa wangu. Naelewa umuhimu wa kubashi¬ri kistaarabu, na nitazidi kuwa mwangalifu na kujidhibiti katika shughuli zangu za kubashiri.
Kwa Watanzania wenzangu, ningependa kuwaelezea hadithi yangu kama ushuhuda wa fursa zilizopo katika michezo ya Premier Bet. Lakini pia, kuwakumbusha kwamba michezo ya kubashiri ni lazima ifanyike kwa uwajibikaji. Furahia msisimko, lakini daima weka ustawi wako mbele na weka mipaka katika shughuli zako za kubashiri. Bashiri kistaarabu.
Kwa mara nyingine tena, nashukuru sana kwa fursa hii kubwa, na nawashukuru sana Premier Bet na jamii nzima ya Watanzania kwa msaada wao wa dhati. Natumai hadithi yangu inaweza kuwahamasisha wengine kufuatilia ndoto zao na kufurahia msisimko wa kubashiri kistaarabu.”
Mchezo wa Navigator wa Premier Casino, unaojulikana kwa kuwa mchezo wenye kuvutia na malipo zaidi, umewateka wachezaji nchini kote. Tukiwa na uchaguzi mkubwa wa michezo ya kuvutia na fursa za kushinda kiasi kikubwa cha pesa kinachobadilisha maisha, Premier Bet inaendelea kubadilisha mandhari ya michezo nchini Tanzania.
Ili kujisajili na kucheza mchezo wa Navigator, tembelea tovuti ya www.premierbet.co.tz.
JE, WEWE NDIYE KIJANA AFUATAE MWENYE BAHATI ZAIDI NCHINI TANZANIA?"