Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Klopp atoa neno kuhusu usajili wa Wirtz Liverpool

Muktasari:

  • Kusajili mchezaji aliyekuwa anawindwa na vilabu vikubwa barani Ulaya ni ushindi mkubwa kwa Liverpool

Liverpool, England. Aliyekuwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amepongeza usajili wa kiungo mshambuliaji, Florian Wirtz, ambaye amekamilisha uhamisho wake kutoka Bayer Leverkusen kwenda Liverpool kwa ada ya rekodi ya pauni milioni 116 Sh400 bilioni za Kitanzania.

Wirtz, 22, alithibitishwa rasmi kuwa mchezaji wa Liverpool siku ya Ijumaa, ikiwa ni sehemu ya harakati za kocha mpya Arne Slot kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu wa pili akiwa Anfield. Kocha huyo wa zamani wa Feyenoord aliiongoza Liverpool kutwaa ubingwa wa Premier League msimu wake wa kwanza na sasa ameanza kujiandaa kwa ushindani mkali zaidi msimu wa 2025/26.

Akizungumza na NTV siku ya Jumamosi, Klopp alifunguka kuhusu usajili huo mkubwa akisema:

“Hii itakuwa ya kipekee kabisa, nina uhakika na hilo. Ni vigumu kuimarisha kikosi kinachotoka kuwa mabingwa, lakini Liverpool wamefanikiwa. Wamepata kipaji cha kipekee kwa kumsajili Florian Wirtz. Ninasubiri kwa hamu kumtazama itakuwa ni burudani kubwa sana,” amesema Klopp.

Wirtz anasifiwa kwa uwezo wa kusoma mchezo, kutoa pasi za hatari na kuunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji. Katika msimu uliopita wa Bundesliga, alifunga mabao 10 na kusaidia mengine 12, akiwa mmoja wa chachu ya mafanikio ya kihistoria ya Leverkusen kutwaa ubingwa bila kupoteza mechi.

Frimpong akutana tena na Wirtz

Wirtz atapata sapoti ya karibu kutoka kwa rafiki yake wa muda mrefu na mchezaji wa zamani wa Leverkusen, Jeremie Frimpong, ambaye pia alisajiliwa na Liverpool mapema mwezi huu. Uhusiano wao wa karibu unatarajiwa kumsaidia Wirtz kuzoea haraka maisha ya Anfield.

“Mimi huwa na Jeremie karibu kila siku nikitoka mazoezini,” amesema Wirtz mwaka jana kauli inayowapa matumaini mashabiki wa Liverpool kuwa kuungana kwao kunaweza kuleta mafanikio zaidi.

Ratiba yenye changamoto kwa Mabingwa watetezi

Liverpool wataanza kampeni yao ya kutetea ubingwa kwa mechi dhidi ya Bournemouth kwenye dimba la Anfield, kabla ya kukutana na Newcastle United ugenini mechi inayotarajiwa kuwa kipimo tosha cha mapema. Katika mwezi wa kwanza wa msimu, kikosi cha Arne Slot pia kitapambana na vigogo kama Arsenal, Everton, Chelsea, na Manchester United kabla ya mwisho wa Oktoba.

Mbali na changamoto za ligi, Liverpool pia watakumbana na pigo la muda litakalosababishwa na Kipute cha Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), kwani nyota wao mkubwa Mohamed Salah atakosa mechi muhimu dhidi ya Arsenal mwezi Januari kwa kuwa atakuwa na kikosi cha Misri.

Kwa upande wa mwisho wa msimu, Liverpool pia watakutana na ratiba ngumu wakicheza dhidi ya Manchester United, Chelsea, Aston Villa na Brentford kwa mpigo. Hii inaongeza msisitizo kwa Slot kuwa na kikosi kipana chenye ubora ili kudhibiti presha ya mashindano ya ndani na kimataifa.

Usajili wa Wirtz

Kusajili mchezaji aliyekuwa anawindwa na vilabu vikubwa barani Ulaya kama Bayern Munich, Real Madrid na Manchester City ni ushindi mkubwa kwa Liverpool. Taarifa kutoka kwa chanzo cha karibu na mchezaji huyo zinaeleza kuwa:

“Florian si mtu wa maneno mengi. Ni mwerevu, hutamka pale anapoona inafaa. Ana utulivu wa kipekee ni mtu ‘cool’.”

Kwa kuzingatia maelezo hayo na ushawishi wa Klopp, Wirtz anaingia katika mazingira yanayomuandalia mafanikio. Ikiwa atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara na kuzoea kasi ya EPL, mashabiki wa Liverpool wana kila sababu ya kutarajia enzi mpya ya mafanikio chini ya Arne Slot