Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wirtz aweka rekodi ya usajili Liverpool

Muktasari:

  • Wirtz anaingia kwenye orodha ya majina makubwa yaliyonunuliwa kwa mamilioni England.

London, England. Pesa, pesa, pesa. Ndio kauli inayozungumzwa kila mahali soka linapotajwa na kwa sasa, jina linalotawala mazungumzo hayo ni Florian Wirtz. Mjerumani huyo mwenye kipaji cha hali ya juu amejiunga na Liverpool kwa ada ya kihistoria ya pauni milioni 116, sawa na shilingi 413 bilioni za Kitanzania, akivunja rekodi zote za usajili ndani ya klabu hiyo kongwe ya Anfield.

Usajili huo haujaishia kutikisa tu Merseyside, bali pia umeamsha matumizi ya pesa kwenye soka la kisasa. Wakati Wirtz anaingia kwenye orodha ya majina makubwa yaliyonunuliwa kwa mamilioni akiwafuata akina Paul Pogba, Jack Grealish, na Declan Rice swali sasa linabaki: Je, usajili huo ulifanikiwa au ulifeli?

Katika uchambuzi wa kina uliofanywa na Mail Sport, klabu zote za Ligi Kuu England zimepimwa kwa kutumia kigezo cha mchezaji wa gharama kubwa zaidi kuwahi kusajiliwa.


Tathmini ya usajili wa gharama kubwa kwa klabu za EPL

Arsenal – Declan Rice (£105m | TZS 341.25 bilioni)

Akiwa ameng’ara West Ham kwa kutwaa Europa Conference League, Rice alijiunga na Arsenal kwa dau la kuvunja rekodi ya klabu. Ameshika nafasi ya kiungo vizuri akifunga mabao na kutoa pasi za mwisho, huku akivutia zaidi kwenye mechi dhidi ya Real Madrid.

Chelsea – Moises Caicedo (£115m | TZS 373.75 bilioni)

Alianza vibaya lakini baadaye akawa mhimili wa safu ya kati ya Chelsea. Ana miaka 23 tu. Bado anayonafasi ya kufanya vizuri zaidi kwenye timu yake.

Liverpool – Darwin Nunez (£85m | TZS 276.25 bilioni)

Alitarajiwa kuwa Haaland mpya. Licha ya kufunga mabao ya maamuzi, alikuwa na makosa mengi. Wirtz sasa amechukua nafasi yake ya kuwa usajili wa bei ghali Anfield.

Manchester City – Jack Grealish (£100m | TZS 325 bilioni)

Ameshinda mataji mengi lakini mchango wake binafsi umebaki kuwa wa kuhojiwa. Aliachwa nje ya kikosi cha Kombe la Dunia la Klabu. Mpaka sasa bado haijajulikana atatua Klabu gani msimu ujao.

Manchester United – Paul Pogba (£100m | TZS 325 bilioni)

Aliuzwa bure na Juventus, akanunuliwa tena kwa gharama kubwa, lakini akashindwa kung’ara kwa kiwango kilichotarajiwa.

Tottenham – Dominic Solanke (£65m | TZS 211.25 bilioni)

Alifunga mabao muhimu lakini msimu uliopita lakini bado hajatosheleza matarajio. Ana nafasi ya kung’ara zaidi msimu ujao.

Wirtz aweka rekodi mpya lakini je, ataleta mafanikio?

Liverpool wameshikilia matumaini makubwa kwa Florian Wirtz nyota mchanga ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika Bundesliga. Lakini historia imetuonyesha kuwa pesa nyingi si dhamana ya mafanikio. Philippe Coutinho, aliyewahi kuuzwa na Liverpool kwa kiasi kikubwa kwenda Barcelona, alishindwa kuonyesha makali yake.

Ni wazi kuwa soka la kisasa limejaa gharama kubwa, lakini klabu nyingi zinaendelea kupoteza fedha bila matokeo yanayoendana na matumizi. Wirtz atahitaji kuonyesha thamani ya uwekezaji huo mkubwa.