Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kabudi aonya wang’oa viti Benjamin Mkapa

Muktasari:

  • Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu itazikutanisha Simba ya Tanzania na RS Berkane.

Dar es Saalam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamaganda Kabudi amewasihi na kuwaonya mashabiki wa soka kutorudia kosa la kung’oa viti katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam na badala yake wawe walinzi wa miundombinu ya uwanja huo.

Kabudi ameyasema hayo leo katika ziara aliyofanya uwanjani hapo kukagua maboresho yake tayari kwa mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Simba na RS Berkane ya Morocco, Mei 25, 2025.

Kabudi amesema kuwa viti vipya vilivyowekwa uwanjani hapo ni bora hivyo mashabiki wanapaswa kuvitunza ili vidumu kwa muda mrefu.

“Mimi nawaomba kabisa tuhimizane ndugu zangu Watanzania wote, watazamaji wote tunaokuja hapa hata tukipata munkari tutunze hii miundombinu hii.

“Hivi viti vipya kabisa hata mimi mwenyewe naviona ni imara,” amesema Kabudi.

Katibu mkuu wa wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo, Gerson Msigwa amesema kuwa uwanja huo upo tayari na kuna kamera kwa ajili ya kunasa watakaoharibu miundombinu hasa viti.

“Sasa hivi hawatoweza kwa sababu tumefunga kamera nyingi. Kila atakayefanya hivyo tutamuona.

“Uwanja upo vizuri na tayari kwa fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya mnyama Simba na RS Berkane ya Morocco, tarehe 25 Mei, 2025.

Mfano wa matukio ya ung’oaji viti katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ni lile la Disemba 15, 2024 ambapo viti 256 viling’olewa katika mechi ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Simba na CS Sfaxien ya Tunisia.

Mchezo huo uliisha kwa timu ya Simba kushinda kwa mabao 2-1, Wekundu wa Msimbazi wakipata bao dakika za jioni (90+) likifungwa na Kibu Denis kitendo kilichowafanya wachezaji na mashabiki wa CS Sfaxien kutoridhishwa na mwamuzi wakionyesha kuamini kwamba mchezo ulikuwa umekwisha na kuanzisha vurugu.

CAF iliipa Simba adhabu ya kucheza mechi moja ya mashindano ya Kombe la Shirikisho pamoja na faini ya fedha kiasi cha Dola 40,000 kwa kosa la mashabiki wake kufanya vurugu hizo.