Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Frank amrithi Postecoglou Spurs

Muktasari:

  • Thomas Frank ameiongoza Brentford katika michezo 317 ambapo ilipata ushindi katika mechi 136, ilitoka sare 71 na kupoteza idadi ya mechi 110 huku ikifunga mabao 527 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 418.

London. Tottenham Hotspur imemtangaza kocha Thomas Frank kuwa meneja wake mkuu kuchukua mikoba ya Age Postecoglou aliyetimuliwa hivi karibuni baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa taji la Europa League.

Frank ambaye alikuwa anainoa Brentford, anajiunga na Spurs kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kukubali ofa aliyowekewa mezani.

“Kwa Thomas tumemteua miongoni mwa makocha wakuu wabunifu na wanaopiga sana hatua kwenye mechi.

“Ana rekodi isiyoacha shaka katika kuendeleza mchezaji na kikosi na tunatazamia aiongoze timu wakati tunajiandaa na msimu ulio mbele,” amesema msemaji wa Spurs.

Mkurugenzi wa soka wa Brentford, Phil Giles ametoa shukrani kwa Frank kwa mchango alioipa klabu hiyo ambayo aliipandisha daraja 2021.

“Ilikuwa jambo zuri kufanya kazi pembeni ya Thomas. Kuanzia nyakati aliyochukua nafasi ya Dean Smith, alifahamu nini tulijaribu kujenga na busara zake, uwezo wa ukocha na akili zake zilisaidia kuipeleka juu klabu.

“Kulikuwa na nyakati nyingi za kipekee na Thomas na hakuna yeyote anayeweza kusahau siku pale Wembley tulipocheza fainali ya mchujo au mechi ya kihisia ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Arsenal,” amesema Giles.

Giles amesema kuwa Brentford haitomsahau Thomas Frank lakini inalazimika kukubaliana na hilo lililotokea.

Kocha huyo ameenda Spurs sambamba na kocha msaidizi Justin Cochrane ambaye aliwahi kuitumikia Tottenham akiwa kocha wa timu ya vijana kwa miaka tisa.

Pia Thomas Frank amepanga kuwavuta kundini kocha wa viungo, Chris Haslam na watathmini wa ubora wa viwango, Joe Newton na Andreas Georgson.

Hao wataungana na makocha wawili ambao Postecoglou amewaacha klabuni hapo ambao ni Matt Wells na Rob Burch.