Fainali kumaliza ubishi Simba, RS Berkane

Muktasari:
- Simba imetinga fainali ya mashindano ya klabu Afrika mara mbili ambapo ya kwanza ilikuwa ni kwenye Kombe la CAF mwaka 1993 na mara ya pili ni msimu huu kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Baada ya kuitoa Stellenbosch ya Afrika Kusini kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba itaumana na RS Berkane ya Morocco katika fainali.
Simba imepita kwa ushindi wa bao 1-0 katika mechi mbili za nusu fainali dhidi ya Stellenbosch baada ya kutoka sare tasa kwenye mechi ya leo Aprili 27, 2025 ugenini huko Afrika Kusini kwenye Uwanja wa Moses Mabhida, Durban, ikibebwa na ushindi iliopata wa bao 1-0 katika mechi ya kwanza Jumapili iliyopita, Aprili 20 katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
RS Berkane licha ya leo kupoteza kwa bao 1-0 ugenini dhidi ya CS Constantine, imetinga fainali kwa ushindi wa mabao 4-1 kwa vile ilipata ushindi nyumbani kwao Morocco wa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza.
Katika fainali, Simba itaanzia ugenini ambapo mechi ya kwanza itachezwa Mei 17 na mechi ya pili itachezwa hapa Tanzania, Mei 25 mwaka huu.
Kukutana kwa Simba na RS Berkane kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu hapana shaka kutamaliza ubishi wa nani zaidi baina yao baada ya hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2021/2022 kumalizika kila upande ukiwa hauna unyonge kwa mwenzake.
Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 ilipocheza mechi ya kwanza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam lililofungwa na Pape Sakho na zilipokutana Morocco, Simba ilifungwa mabao 2-0.
Timu hizo zilimaliza kila moja ikiwa na pointi 10 lakini Berkane iliongoza msimamo wa kundi D kwa vile ilibebwa na kanuni ya kupata matokeo mazuri katika mechi mbili baina yao