Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAF yamuondoa Arajiga Kariakoo Derby

Muktasari:

  • Mchezo wa mwisho wa Simba na Yanga kuchezeshwa na Ahmed Arajiga ulikuwa ni wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kuna uwezekano finyu kwa refa Ahmed Arajiga kuchezesha mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba ‘Kariakoo Derby’, Jumatano, Juni 25, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Arajiga yupo Cairo, Misri akishiriki kozi ya maandalizi kwa marefa kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 zitakazofanyika Agosti 2 hadi Agosti 30 mwaka huu katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania .

Kozi hiyo ya marefa ilianza Alhamisi Juni 21 na itamalizika Jumatano, Juni 25 mwaka huu ikiwajumuisha marefa Idadi ya marefa 58 kutoka nchi mbalimbali. Arajiga yupo katika kundi la marefa wa kati 29 walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kushiriki kozi hiyo ya maandalizi ya CHAN.

Ukiondoa Arajiga Tanzania ina marefa wengine wawili katika kozi hiyo ambao ni Frank Komba na Hamdani Said ambao wapo katika kundi la marefa wasaidizi. Ikumbukwe Arajiga ndiye alipangwa kuchezesha mechi ya Yanga na Simba, Machi 8 mwaka huu.

Arajiga alipangwa kuchezesha mechi hiyo akisaidiwa na Mohamed Mkono na Kassim Mpanga huku refa wa akiba akiwa ni Amina Kyando.

Katika kozi hiyo ya maandalizi ya CHAN 2024 inayoendelea Misri, Marefa wa kati na nchi zao kwenye mabano ni Hamza El Fariq na Kech Mustapha (Morocco), Jean Ouattara na Vincent Kabore (Burkina Faso), Houssam Benyahya na Loutfi Bekouassa (Algeria), Adissa Ligali (Benin), Mohamed Athoumani (Comoros), Messie Nvoulou (Congo), Kpan Franklin (Ivory Coast), Kabanga Yannick (DR Congo), Tsegay Mogos (Eritrea), Ahmed Mahmoud (Misri), Jammeh Lamin (Gambia), Dickens Mimisa (Kenya), Ahmed Abdulrazg (Libya) na Rakotojaona

Andofetra (Madagascar).

Wengine ni Diakhate Ousmane (Mali), Milazare Patrice (Mauritius), Diouf Adalbert (Senegal), Jerry Chavani (Afrika Kusini), Arajiga (Tanzania), Aklesso Gnama (Togo), Melki Mehrez (Tunisia), Lucky Kasalirwe (Uganda), Celso Alvacao (Msumbiji), Brahamou Ali (Niger), Brighton Chimene (Zimbabwe) na Mefire Abdel (Cameroon).

Waamuzi wasaidizi

Bouzit (Algeria), Ngila Bongele (DR Congo), Lucky Kegalogetswe (Botswana), Sanou Oumar (Burkina Faso), Emery Niyongabo (Burundi),

Menye Mpele (Cameroon), Amaldine Soulaimane (Comoros), Alao Salim (Benin), Fasika Biru (Ethiopia), Jawo Aziz (Gambia) na Addy Dodoo (Ghana).

Wapo pia Mwangi Kuria (Kenya), Joel Doe (Liberia), Diba Hamedine (Mauritania), Nassiri Hamza (Morocco), Yacouba Aziz (Niger), Dieudonne Mutuyimana (Rwanda), Omer Ahmed (Sudan), Frank Komba na Hamdani Said (Tanzania) na Wael Hanachi (Tunisia).