Bendera ya ligi yetu ilivyopepea Morocco
Makala ya 35 ya mashindano ya soka kutafuta taifa bingwa barani Afrika, AFCON 2025, yanaendelea huko Morocco katika viwanja nane tofauti.
Jumla ya maataifa 24 yameshiriki huku kila moja likitakiwa kuwa na wachezaji 28. Hii ina maana kwamba jumla ya wachezaji 672 wameshiriki. Wachezaji hawa ni kutoka ligi mbalimbali duniani, za madaraja tofauti. Mpangilio wa idadi ya wachezaji na ligi zao ni kama ifuatavyo
- Ufaransa: 79 (11.9%)
- England: 50 (7.53%)
- Afrika Kusini: 32 (4.82%)
- Misri: 31 (4.67%)
- Hispania: 29 (4.37%)
- Uturuki: 28 (4.22%)
- Italia: 26 (3.92%)
- Tanzania: 25 (3.77%)
- Ujerumani: 21 (3.16%)
- Botswana: 21 (3.16%)
Ligi ya Tanzania inashika nafasi ya tatu kwa ligi za Afrika zilizotoa wachezaji wengi kwenye AFCON hii, nyuma ya Misri na Afrika Kusini tu. Hili ni jambo la kujipongeza sana kwa sababu inaonesha kwamba ligi yetu ni bora na imara.
Ukiacha wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, kuna wengine kadhaa kutoka mataifa mengine wapo huko.
Djigui Diarra - Yanga (Mali)
Khalid Aucho - Singida Black Stars (Uganda)
Prince Dube - Yanga (Zimbabwe)
Steven Mukwala - Simba (Uganda)
Zaidi ya wachezaji, kuna watu wengine kama Riedoh Berdien wa Simba ambaye ni kocha wa viungo wa Burkina Faso. Pia kuna wale ambao kwa sasa hawapo Tanzania, lakini waliwahi kuwa hapa nchini.
Wachezaji
Fiston Mayele (DRC) - alikuwa Yanga 2021 - 2023.
Che Malone (Cameroon) alikuwa Simba 2023 - 2025.
Aziz Ki (Burkina Faso) alikuwa Yanga 2022 - 2025.
Kennedy Musonda (Zambia) - alikuwa Simba 2023 - 2025.
Makocha
Mario Marinika - kocha mkuu Zimbabwe, alikuwa Azam kocha msaidizi wa Azam FC msimu wa 2015/16.
Thom Saintfiet - kocha mkuu Mali, alikuwa Yanga mwaka 2012.
Chlouha Zakaria - Kocha wa makipa wa Morocco, alikuwa kocha wa makipa wa Simba 2024/25.
AFCON 1980 LAGOS NIGERIA
Tanzania ilifuzu kwa mara ya kwanza kushiriki AFCON ya 1980 iliyofanyika Lagos Nigeria.
Hapa ndio ilikuwa mara ya kwanza lifi ya Tanzania kuwakilishwa.
Kikosi chote cha Stars kilijaa wachezaji kutoka ligi yetu.
Athuman Mambosasa - Nyota Morogoro
Leopold 'Tasso' Mukebezi - Balimi FC Kagera
Mohamed 'Machela' Kajole - Simba SC
Leodeger Tenga - Pan Africa
Jellah Mtagwa - Pan Africa
Juma Mkambi - Nyota Mtwara
Omary Hussein 'Keagan' - Yanga
Hussein Ngurungu - Nyota Nyekundu
Peter Tino - African Sports Tanga
Mohamed 'Adolf' Rishard - Pan Africa
Thuwen Waziri Ally - Simba SC
Juma Pondamali - Pan Africa
Idd Pazi - Majimaji Songea
Daud Salum 'Bruce Lee' - Simba SC
Ahmad Amasha - Tumbaku Morogoro
Salim Amir - Coastal Union
Rashid Idd Chama - Yanga
Mtemi Ramadhan - Majimaji
Willy Kiango - Coastal Union
Mohamed Salim - Coastal Union
AFCON 2017 GABON
Baada ya 1980, ligi ya Tanzania haikuwakilishwa tena kwenye AFCON hadi 2017 pale ligi ya Tanzania ilipowakilishwa na wachezaji wawili.
Juuko Murshid wa Simba aliyeshiriki akiwa na taifa lake la Uganda.
Na Bruce Kangwa wa Azam FC aliyeshiriki na taifa lake la Zimbabwe.
Hii ilikuwa AFCON iliyofanyika nchini Gabon. Awali ilipangwa kufanyika Libya lakini vita vya wenyewe kwa wenyewe vikailazimu CAF kuhamisha mashindano.
AFCON 2019 MISRI
Tanzania ilifuzu kwa mara ya kwanza baada ya takribani miaka 40, na kwenda na wachezaji 15 kutoka ligi ya ndani
Aishi Manula - Simba SC.
Metacha Mnata - Mbao FC.
Aron Kalambo - Tz Prisons.
Vicent Philipo - Mbao FC.
Gadiel Michael - Yanga SC.
Ally Mtoni - Lipuli FC.
Mohamed Hussein - Simba SC.
David Mwantika - Azam FC
Kelvin Yondan - Yanga
Erasto Nyoni - Simba SC.
Feisal Salum - Yanga SC.
Mudathir Yahya - Azam FC.
Frank Domayo – Azam FC
John Bocco – Simba SC.
Pia walikuwepo wengine watatu kutoka timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.
Emmauel Okwi - Simba SC
Juuko Murshid - Simba SC
Nicholas Wadada - Azam FC
Na pia alikuwepo Thaban Kamusoko wa Yanga akiiwakilisha Zimbabwe.
AFCON 2021 CAMEROON
Safari hii ligi ya Tanzania iliwakilishwa na wachezaji watatu wa Zimbabwe kutoka Azam FC.
Bruce Kangwa
Prince Dube
Never Tigere
AFCON 2023
Tanzania ilifuzu tena safari hii na kuchukua wachezaji 11 kutoka ligi ya nyumbani.
Mudathir Yahya - Yanga
Ibrahim Hamad - Yanga
Dickson Job - Yanga
Feisal Salum - Azam FC
Bakari Mwamnyeto - Yanga
Beno Kakolanya - Singida Black Stars
Mohamed Hussein - Simba FC
Sospeter Bajana - Azam FC
Lusajo Mwaikenda - Azam FC
Aishi Manula - Simba
Mzamiru Yassin - Simba
Kibu Denis - Simba
Abdulmalik Zakaria- Namungo
Lakini pia kulikuwa na wengine kutoka mataifa tofauti wakicheza Tanzania.
Stephane Aziz Ki wa Yanga alikuwa na Burkina Faso.
Djigui Diarra wa Yanga alikuwa na Mali.
Henock Inonga wa Simba alikuwa na DRC.
Na Zambia ilikuwa na wawili, Clatous Chama wa Simba na Kennedy Musonda wa Yanga.
Baeki wa Taifa Stars, Bakar Nondo akijaribu kumtoka beki a Morocoo, Noussair Mazraoui. Picha na Mtandao
Hitimisho
Ligi ya Tanzania inatajwa kama moja ya ligi bora barani Afrika, mambo kama.haya ndio ushahidi.
Unapokuwa na ligi ambayo wachezaji wake wanategemewa na mataifa yaliyopiga hatua kwa kuzalisha vipaji vikubwa, maana yake una kitu.
Na haya yote yameanza 2017, mwaka ambao Wallace Karia alianza kuwa Rais wa TFF.
Sasa Tanzania inafuzu AFCON bila shida. Klabu zale zinafuzu hatua ya makundi bila shida.
Na wachezaji wanaocheza Tanzania wanazitumikia nchi kubwa bila shida
Hapana shaka kwamba ligi yetu ni ligi bora hasa.