Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta kumvuta mshambuliaji mpya Arsenal

Arsenal Pict

Muktasari:

  • Arsenal imekuwa na uhitaji mkubwa wa kuboresha safu yao ya ushambuliaji kwenye uhamisho wa dirisha hili la Januari baada ya washambuliaji wake Bukayo Saka na Gabriel Jesus kuwa majeruhi.

LONDON, ENGLAND: Mikel Arteta amesema Arsenal ipo tayari kuleta kwenye kikosi chao fowadi mpya dirisha la majira ya kiangazi na dili hilo watalikamilisha mwezi huu.

Arsenal imekuwa na uhitaji mkubwa wa kuboresha safu yao ya ushambuliaji kwenye uhamisho wa dirisha hili la Januari baada ya washambuliaji wake Bukayo Saka na Gabriel Jesus kuwa majeruhi.

Straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, 21, amekuwa akihusishwa sana na miamba hiyo ya Emirates kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Sesko anatarajia kuachana na miamba hiyo ya Ujerumani kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwisho wa msimu huu.

Lakini, Arsenal italazimika kutoa Pauni 70 milioni kunasa saini ya straika huyo wa Slovenia kwa dili la muda mrefu la kama itahitaji kwa mkopo.

Kocha Arteta alisema: “Tunaona ulazima huo kwa sasa kutokana na kilichotokea kwa wiki chache zilizopita.

“Hatukuwa na mpango kabisa kwenye dirisha hili. Sasa itabidi tuwe na mpango, tukitazama kikosi chetu, tutaangalia namna ya kulitumia dirisha na tutaangalia pia kwenye akademia yetu. Tumepoteza wachezaji wawili muhimu wa pale mbele, hivyo tunahitaji kuboresha kwenye lile eneo.”

Saka amefanyiwa upasuaji kabla ya Krismasi na atakuwa nje ya uwanja hadi Machi, wakati Jesus atakosa mwaka wote huu kutokana na kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli ya goti.

Wakala wa Sesko, Elvis Basanovic alikiri uhamisho wa Januari kwa mteja wake unaweza usitokee labda kama tu kutakuwa na ofa ya maana italetwe, huku Leipzig wanapambana kuwania nafasi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Arteta aliongeza: “Kwa kila mchezaji, ni lazima ufahamu wazi viwango vyaka. Ni mchezaji gani unamsajili? Unatarajia nini? Huyo mchezaji atakwenda kufiti vipi kwenye kikosi chako?”


MAVITU YA SESKO LEIPZIG 2024-25

-Amecheza: Mechi 17

-Ametengeneza: Nafasi 7

-Amefunga: Mabao 8

-Ametoa: Asisti 2

-Amelenga goli: Mashuti 17

-Amegonga: Pasi 315