Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Martinez aingia anga za Chelsea

Muktasari:

  • Chelsea inaamini kwamba ikimpata Martinez anaweza kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo ina wachezaji kama Noni Madueke, Nicolas Jackson na Christopher Nkunku.

Inaelezwa kwamba Chelsea imeingia sokoni kutafuta mshambuliaji huku ikimtolea macho nahodha wa Inter Milan, Lautaro Martinez ambaye ametoka kuongeza mkataba wa miaka mitano hivi karibuni kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya Italia.

Chelsea imepanga kupeleka ofa ikiambatanisha na wachezaji watatu ambao ni Benoit Badiashile, Carney Chukwuemeka na Mykhailo Mudryk ambao kocha wa Chelsea, Enzo Maresca hajavutiwa kufanya nao kazi.

Kuambatanishwa kwa Mudryk kuwa miongoni mwa wachezaji watatu ambao Chelsea inataka kufanya mabadilishano, inaweza kuwapa wakati mgumu viongozi wa Inter Milan kutokana na mchezaji huyo kusimamishwa kucheza England kwa kile kinachodaiwa anatumia dawa za kusisimua misuli.

Chelsea inaamini kwamba ikimpata Martinez anaweza kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo ina wachezaji kama Noni Madueke, Nicolas Jackson na Christopher Nkunku.

Hata hivyo, Martinez amekuwa na wakati mgumu hivi karibuni huku akipambana kurejea kwenye ubora wake wa kufumania nyavu ambapo msimu huu amecheza mechi 21 akifunga mabao sita katika michuano tofauti. Msimu uliopita alifunga mabao 27 kwenye mechi 44.

Katika kikosi cha Inter Milan, kinara wa ufungaji ni Marcus Thuram ambaye amefunga mabao 12 kwenye mechi 17 za Seria A akiwa pia ndiye anayeongoza kwenye orodha ya wafungaji bora Seria A sawa na Mateo Retegui wa Atalanta.

Licha ya kiwango chake kushuka, bado Inter Milan haionyeshi nia ya kuachana na Martinez ambaye ni kipenzi cha mashabiki wengi wa klabu hiyo ambao walimuimbia nyimbo za kumfariji alipokuwa akifanyiwa mabadiliko kwenye mchezo wa Serie A dhidi ya Como uliopigwa Desemba 23, 2024 kwenye Dimba la Giuseppe Meazza.