Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yaendeleza ubabe, Man United, Chelsea hoi

Muktasari:

  • Katika mchezo huo, Alexis Mac Allister alitengeneza mabao mawili yaliyofungwa na Gakpo na Jones, wakati Gakpo naye licha ya kufunga, alimtengenezea bao Salah.

Liverpool, England. Liverpool imeendelea kupata matokeo mazuri katika Ligi Kuu England baada ya kuichapa Leicester City mabao 3-1, mchezo uliochezwa jana Desemba 26, 2024 kwenye Uwanja wa Anfield.

Leicester ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya sita kupitia Jordan Ayew akimalizia pasi ya Stephy Mavididi, kabla ya Cody Gakpo kuisawazishia Liverpool dakika ya 45+1.

Mabao mengine ya Liverpool yalifungwa na Curtis Jones dakika ya 49 na Mohamed Salah akahitimisha ushindi huo kwa bao la dakika ya 82.

Katika mchezo huo, Alexis Mac Allister alitengeneza mabao mawili yaliyofungwa na Gakpo na Jones, wakati Gakpo naye licha ya kufunga, alimtengenezea bao Salah.

Matokeo hayo yanazidi kuiweka pazuri Liverpool ikifikisha pointi 42 na kujikita zaidi kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya pointi saba dhidi ya Chelsea inayoshika nafasi ya pili.

Mbali na hilo, bao alilofunga Salah linamfanya afikishe mabao 100 aliyofunga uwanja wa nyumbani kwenye Premier ambapo 98 ameyafungia Anfield akiitumikia Liverpool na mawili aliyafunga Stanford Bridge alipokuwa Chelsea.

Wakati Liverpool ikitakata, Chelsea ikiwa nyumbani imepunguzwa kasi baada ya kufungwa mabao 1-2 dhidi ya Fulham kwenye Uwanja wa Stanford Bridge huku ikisalia na pointi 35 katika nafasi ya pili.

Manchester United chini ya Ruben Amorim, nayo ilipoteza kwa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Wolverhampton huku kiungo wake Bruno Fernandes akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 47 akiwa ni mchezaji wa kwanza kutolewa mchezoni mara tatu ndani ya msimu mmoja tangu alipofanya hivyo Nemanja Vidic msimu wa 2008-2009.

Wachezaji wengine waliyoonyeshwa kadi nyekundu kwenye michezo ya jana ni Djed Spence ambaye ni beki wa kulia wa Tottenham pamoja na mshambuliaji wa Aston Villa, Jhon Durán.

Manchester City ya Pep Guardiola imeendelea na upepo mbaya wa kukosa matokeo mazuri baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 ikiwa nyumbani dhidi ya Everton huku Erling Haaland akikosa penalti dakika ya 53. Kwenye mechi 12 zilizopita michuano tofauti, Man City imepata ushindi moja, imefungwa tisa huku ikipata sare mbili.

Baada ya mchezo kumalizika, Guardiola amesema: "Ikiwa tutaweza, tutaongeza wachezaji kwenye dirisha dogo la Januari, tumekuwa na safu mbaya ya ulinzi pamoja na viungo wa kati, ni lazima tuongeze wachezaji."

Manchester City inatarajia kuongeza wachezaji baada ya kuwa na mwenendo mbaya msimu huu huku majeruhi wakitajwa kama sababu ambapo wapo mbioni kumvuta bwana mdogo kutoka River Plate ya Argentina, Claudio Echeverri.

Michezo mingine ya EPL itapigwa tena leo ambapo Arsenal itakuwa nyumbani dhidi ya Ipswich Town ambapo vijana hao wa Mikel Arteta kama wakishinda watapanda nafasi kutoka ya nne hadi ya pili kwa kufikisha pointi 36. Mechi nyingine ni Brentford itakuwa ugenini dhidi ya Brighton.


MATOKEO YA MECHI ZILIZOPIGWA JANA EPL

Man City 1-1 Everton

Bournemouth 0-0 Crystal Palace

Chelsea  1-2 Fulham

Newcastle 3-0 Aston Villa

Southampton 0-1 West Ham

Wolverhampton 2-0 Man United

Liverpool 3-1 Leicester

Nottingham Forest 1-0 Tottenham