Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Lumumba’ kuikosa DR Congo dhidi ya Jamaica kisa viza

Shabiki maarufu wa DR Congo, Michel Kuka Mboladinga  maarufu kama Lumumba. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Mboladinga alijijengea umaarufu katika Fainali za AFCON 2025 nchini Morocco ambapo alikuwa akiigiza staili ya usimamaji ya Waziri Mkuu wa zamani wa DR Congo, Patrice Lumumba.

Shabiki maarufu wa DR Congo, Michel Kuka Mboladinga ‘Lumumba’ hatoonekana uwanjani baadaye kuanzia saa 6:00 katika mchezo baina ya DR Congo na Jamaica, jijini Guadarajala  Mexico katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Mboladinga ambaye amejijengea umaarufu mkubwa kwa kumuigilizia Waziri Mkuu wa zamani wa DR Congo, Patrice Lumumba, ameshindwa kusafiri kwenda Mexico yeye na baadhi ya mashabiki wenzake kutokana na kukosa viza ya kuingilia nchini humo.

Shabiki huyo na wenzake wamekwamia nchini Kenya uliko ubalozi wa Mexico ambako walifika kujaribu kuomba viza za kwenda nchini humo kwa ajili ya mchezo huo muhimu wa baadaye wa hatua ya mchujo.

Licha ya jitihada za serikali ya DR Congo kuhakikisha Mboladinga na wenzake wanafanikiwa kusafiri kuungana na timu yao, Mexico imeshindwa kuwapa viza mashabiki hao na hivyo watatazama mechi wakiwa majumbani.

Mbolandinga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X amethibitisha kwamba hatohudhuria mchezo huo wa leo.

“Ninasikitika sana kuwajulisha kwamba sitakuwa nchini Mexico. Tulikuwa Kenya, lakini licha ya juhudi zote zilizofanywa, hasa na Waziri wa Michezo, Mheshimiwa Didier Budimbu, hatukuweza kupata viza.

“Hivyo tulirejea Kinshasa pamoja na watangazaji wenzangu asubuhi ya Jumapili, Machi 29,” ameandika Mbolandinga.

Ilikuwa imeripotiwa hapo awali kwamba DR Congo ilikumbwa na matatizo ya viza kabla ya mechi yao ya mchujo wa mabara kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026 huko Guadalajara, Mexico.

Kulikuwa na ucheleweshaji katika kuidhinishwa kwa viza za wachezaji, na ilidhaniwa kwamba hali hiyo ingeweza kuathiri maandalizi yao, lakini ilitatuliwa kwa wakati ili wachezaji waweze kusafiri.

Ushindi katika mchezo wa baadaye utaifanya DR Congo iungane na mataifa mengine tisa ya Afrika kushiriki Fainali za Kombe la Dunia huko Marekani, Canada na Mexico, kuanzia Juni 11, 2026.

DR Congo ikiwa itafuzu itakuwa imemaliza ukame wa miaka 52 wa kukaa bila kushiriki fainali hizo tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1974.