Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katibu Mkuu CAF ajiuzulu, mrithi wake atajwa

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, Veron Mosengo-Omba. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Raia huyo wa DR Congo amejiuzulu nafasi yake baada ya kuitumikia CAF kwa miaka mitano tangu 2021 alipoteuliwa na shirikisho hilo akitokea FIFA ambako alikuwa Mkuu wa Idara ya Vyama na Mashirikisho wanachama.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, Veron Mosengo-Omba ameng’atuka katika nafasi yake baada ya leo, Jumapili, Mei 29, kuanika hadharani uamuzi wake.

Kujiuzulu kwa Mosengo-Omba kuhitimisha kipindi cha uongozi wake kilichoambatana na mageuzi makubwa pamoja na kuongezeka kwa mijadala yenye utata kuhusu masuala ya uongozi ndani ya chombo kinachosimamia soka la Afrika.

“Baada ya zaidi ya miaka 30 ya taaluma ya kimataifa niliyoiweka katika kuendeleza dhana bora ya soka inayowaunganisha watu, kuelimisha, na kuunda fursa za matumaini, nimeamua kuachia nafasi yangu kama Katibu Mkuu wa CAF ili nijikite katika miradi yangu binafsi,” amesema Mosengo-Omba.

Raia huyo wa DR Congo amejiuzulu nafasi yake baada ya kuitumikia CAF kwa miaka mitano tangu 2021 alipoteuliwa na shirikisho hilo akitokea FIFA ambako alikuwa Mkuu wa Idara ya Vyama na Mashirikisho wanachama.

Kujiuzulu kwa Mosengo-Omba kumekuja katika kipindi ambacho CAF imekuwa ikituhumiwa kwa upendeleo, ubaguzi na rushwa hasa baada ya uamuzi wa shirikisho hilo kuivua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuitangaza Morocco kuwa mshindi.

Muda mfupi baada ya Mosengo-Omba kujiuzulu, CAF imemtangaza Mkurugenzi wake wa Mashindano, Samson Adamu kuwa Kaimu Katibu Mkuu.

Uamuzi huo ambao umetangazwa na Rais wa CAF, Patrice Motsepe, unaashiria mabadiliko makubwa katika uongozi wa chombo hicho kinachosimamia soka la Afrika.

Adamu anakuwa Mnigeria wa kwanza kushika nafasi ya juu zaidi ya kiutawala ndani ya CAF.

Kabla ya kuteuliwa, Adamu alikuwa anatajwa kuwa miongoni mwa watu wa kushika kwa kudumu nafasi hiyo, na ataanza kazi hiyo mara moja.

Uteuzi wake unaonekana na wadau wa sekta hiyo kama hatua ya kimkakati ya kuhakikisha mwendelezo wa shughuli za kiutendaji wakati CAF inajiandaa kalenda ya shughuli nyingi za mashindano na mageuzi ya kimuundo.

Katika nafasi yake mpya, Adamu atasimamia shughuli za kila siku za utawala wa shirikisho hilo, akisimamia sekretarieti na kuratibu utekelezaji wa maamuzi yanayofanywa na Kamati ya Utendaji.

Historia ya kitaaluma na kiutawala ya Adamu inaongezewa nguvu zaidi na msingi wake wa hali ya juu wa elimu. Akiwa mhitimu wa programu mashuhuri ya FIFA Master, ana shahada katika Usimamizi wa Biashara na Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Marekani cha Paris.

Kipindi chake kama Mkurugenzi wa Mashindano, kilichoanza mwaka 2018, kilimshuhudia akisimamia karibu mashindano 30 tofauti ya Afrika.