Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni mwaka wa uamuzi, wanawake jitokezeni kugombea nafasi za uongozi

Muktasari:

  • Hivyo wakati tunahubiri uongozi katika nyanja ya 50 kwa 50, naendelea kusisitiza kuwa mwaka huu unapaswa kutumika vema kwa wanawake kubadili mitazamo na wajitokeze kuomba nafasi hizo. Ni wakati wa kubadilika.

Mwaka 2025 ni mwaka muhimu kwa mustakabali wa taifa la Tanzania,  ni mwaka wa uchaguzi mkuu ambao utatoa mwelekeo mpya wa kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa miaka mingine mitano ijayo.

Katika kipindi hiki, ndicho ambacho Watanzania Bara na Visiwani hupata nafasi ya kuwachagua viongozi watakaosimamia rasilimali, kuunda sera na kusimamia utekelezaji wa maendeleo katika maeneo yao.

Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha kuwa mara nyingi wanawake huonekana wakiwa nyuma katika ushindani wa nafasi hizi muhimu.

Ingawa hali si mbaya sana ikilinganishwa na miaka kadhaa ya uchaguzi iliyopita, bado wanawake na wasichana wenye sifa, hujikuta wakibaki kuwa watazamaji au kuwapigia debe na kura wake wenye jinsi ya kiume.

Kama nilivyoeleza hapo juu, bado hali hairidhishi ya idadi ya wanawake na wasichana wanaojitokeza kuomba nafasi hizo kupitia majimbo na kata za uchaguzi.

Hivyo wakati tunahubiri uongozi katika nyanja ya 50 kwa 50, naendelea kusisitiza kuwa mwaka huu unapaswa kutumika vema kwa wanawake kubadili mitazamo na wajitokeze kuomba nafasi hizo. Ni wakati wa kubadilika.

Wanawake wanapaswa kusimama na kusema "Tupo, Tunaweza na Tunastahili." Takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa idadi ya wanawake wanaojitokeza kugombea nafasi za udiwani na ubunge bado ni ndogo kulinganisha na wanaume, licha ya uwepo wa sera na mikakati ya kuwawezesha wanawake kisiasa.

Zipo sbabu kadhaa zinatajwa kuwa ni kikwazo kwao ikiwamo ya hofu ya kuonekana hawana uwezo, kukosa uungwaji mkono wa kifamilia au kijamii, hali ya duni kiuchumi sambamba na hofu ya kukabiliana na mazingira ya kisiasa yenye changamoto kama vile matusi, kejeli na dhuluma.

Lakini historia inaonyesha kuwa pale wanawake wanapopewa nafasi, wanafanya kazi kwa ufanisi, kwa uadilifu na kwa kujali maslahi ya wengi.

Ninayo mifano hai ya viongozi wanawake walioleta mabadiliko chanya katika maeneo yao, kutoka ngazi ya mtaa hadi taifa.

Hii ni fursa kwa wanawake kutumia haki yao ya kikatiba sio tu kupiga kura, bali pia kugombea uongozi.

Ili sauti ya wanawake isikike vyema bungeni, kwenye halmashauri na kwenye vyombo vya uamuzi, ni wakati wa wanawake wenyewe sasa kuwa sehemu ya uundaji wa uamuzi huo.

Aliwahi kusema mara kadhaa, mama muasisi wa mkutano wa Beijing, Getrude Mongela kuwa, Kama wanawake hawatashiriki kwa kiwango kikubwa katika kugombea nafasi za uongozi, watabaki kuwa watazamaji wa sera na uamuzi unaowahusu moja kwa moja.

Nami nipende kusisitiza katika hilo kwamba, wanawake, wsichana, msisubiri kupewa, ni wakati wa kushiriki uchaguzi kikamilifu.

Wanawake wa Tanzania kwa umoja wenu, lazima mseme kwa lugha moja kwamba ni wajibu wenu kuomba ridhaa kwa wananchi kama wafanyavyo wanaume.

Simameni. Jitokezeni. Ombeni nafasi hizo. Mnao uwezo, uzoefu na maono ya kuleta mageuzi kwenye maeneo yenu.

Mashirika ya kiraia, vyama vya siasa na taasisi za kijamii zipo tayari kuwasaidia kupitia mafunzo, ushauri na mitandao ya uungwaji mkono. Wanawake wasisite kugombea, hata kama wanajua changamoto ni kubwa, kwa sababu mabadiliko huletwa na wale wanaothubutu.

Kwa hiyo, mwaka huu msibaki nyuma tena, msisubiri tu siku ya kupiga kura, bali mchukue hatua leo, muda ukifika chukuenia fomu za kuomba ridhaa kuanzia kwenye mchakato ndani ya vyama vyenu vya siasa.

Wapo ambao wanonekana wazi kwamba uwezo wa kuongoza wanao, lakini wanaogpa kuthubutu, wahimizwe na kuhamasishwe wasibaki nyuma.

0755466690