Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Heche: Hatupaswi kuwa maskini, nchini ina rasilimali za kutosha

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema Tanzania ni nchi kubwa yenye kilomita za mraba zaidi ya 945,000 yenye utajiri wa rasilimali ikiwemo madini, mbuga za wanyama, mito, maziwa, mlima mrefu na gesi.

Kutokana na utajiri huo chama hicho kimesema wananchi wa Tanzania hawapaswi kuteseka kwa umaskini. 

Hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Ifakara, Wilaya ya Kilombero jimbo la Mlimba mkoani Morogoro, ikiwa ni siku ya kwanza ya kampeni ya 'No reforms, no election' katika mikoa ya Kanda ya Kati inayoanza leo Juni 5, 2025.

“Hatupaswi kuwa maskini ndio maana tunataka mabadiliko ya sheria za uchaguzi ili tupate viongozi wenye maono ambao hawatafanya tuwe maskini,” amesema Heche.

Heche pamoja na viongozi wengine wa juu wa Chadema wanafanya ziara kwenye mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida inayounda Kanda ya Kati ya chama hicho.

“Lazima tulinde rasilimali za nchi yetu, tulinde ajira zetu, tutengeneze uchumi wa ndani kwa kuwa na viwanda vitakavyozalisha ajira ambapo pesa itazunguka ndani ya nchi,” amesema Heche.

Katika mkutano huo Heche amesema: “Nakimbiaje uchaguzi nimekuwa diwani nikiwa mwanafunzi, nimekuwa mbunge kabla sina hata mwanamke, nakimbiaje uchaguzi mimi, naujua utamu wa Bunge na nikiwa huko najenga hoja.”

“Ndio maana tunataka uchaguzi huru na haki Samia (Suluhu Hassan-Rais wa Tanzania) asimame hapa (Tundu) Lissu (mwenyekiti wa Chadema) hapa kipigwe dakika 90 wananchi waamue.”

Katika mikutano hiyo Heche akiwa na viongozi wengine wa chama hicho kwenye ziara hiyo atafanya mikutano ya hadhara kuelimisha na kushawishi umma kuunga mkono msimamo kampeni ya kudai mabadiliko ya sheria na mfumo wa uchaguzi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Deogratius Mahinyila amesema vijana wana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko kwa kuwa wako wengi nchini.

Naye mjumbe mteule wa Kamati Kuu, Rose Mayemba amesema uamuzi ya chama hicho wa kutaka mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi unapaswa kuungwa mkono na wananchi wote wakiwamo wa Kilombero.