Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chaumma waja na vipaumbele vitatu

Mgombea wa urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe akiwahutubia wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho uliofanyika Manzese jijini Dar es Salaam jana.  Picha na Omar Fungo

Muktasari:

Akizindua kampeni za chama hicho jana katika Uwanja wa Bakhresa Manzese jana, Rungwe alisema akichaguliwa atabadilisha maisha ya Watanzania kuwa bora.

Dar es Salaam. Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe ameahidi vipaumbele vitatu, ajira, afya bure na elimu kwa Watanzania wote endapo atachaguliwa kuongoza nchi.

Akizindua kampeni za chama hicho jana katika Uwanja wa Bakhresa Manzese jana, Rungwe alisema akichaguliwa atabadilisha maisha ya Watanzania kuwa bora.

“Kama una nguvu za kufanya kazi utafanya kazi na kupata kipato, kazi zitakuwepo hata kama umestaafu kama una nguvu utafanya kazi kwa sababu hata wastaafu wana hitaji fedha ili waishi,” alisema Rungwe.

Alisema ili kutekeleza hilo, atajenga pia viwanda vyenye kutumia malighafi zinazopatikana nchini.

Akitolea mfano, alisema Tanzania ni ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya ng’ombe barani Afrika, ikitanguliwa na Ethiopia, lakini haina viwanda vya kusindika nyama, maziwa na ngozi.

“Nikiingia Ikulu nitahakikisha ninajenga viwanda vya kusindika nyama, maziwa na ngozi ili kuuza bidhaa hizo nje na kutoa ajira kwa wananchi,” alisema mgombea huyo.

Alisema ili kuongeza wigo wa ajira, atahakikisha anaboresha kilimo kwa kuuza matrekta na mashine nyingine za kilimo kwa bei nafuu ziweze kutumiwa na wakulima na hivyo kuwarahisishia kazi.

Afya

Alisema ataboresha mazingira ya upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya afya na hospitali kwa kuwa kero hiyo imekuwa sugu nchini.

Alisema tatizo la uhaba wa dawa katika hospitali za Serikali ni kubwa, lakini inashangaza kuona kwenye maduka yaliyo karibu na hospitali hizo kila aina ya dawa zinapatikana.

Elimu

Rungwe alisema ataboresha elimu ili kuhakikisha kila Mtanzania anasoma na kupatiwa huduma zote zilizokuwa zinapatikana katika Serikali ya Awamu ya Kwanza. Chama cha Ukombozi wa Umma

Mgombea Mwenza wa chama hicho, Issa Abbas Hussein alisema anashangaa watoto wanapoanza darasa la kwanza wanachangishwa fedha za madawati, lakini wanakaa chini.

“Hizi fedha za michango ya madawati itaisha lini kwa watoto wetu, kibaya zaidi wanachangishwa kila wanapoingia darasa la kwanza, lakini madawati hayanunuliwi, tupeni nchi tuwakomeshe mafisadi hawa wanaoshibisha matumbo yao tu,” alisema.

Hussein.

Katika mkutano huo ulioanza saa 9.00 hadi saa 12.00 jioni, mmoja wa wananchi aliyekuwa amevalia kofia ya CCM aliondolewa mzobemzobe na wafuasi wa chama hicho kwa madai kuwa ya kuwa alikuwa mkutanoni hapo kwa lengo la kuwahujumu. Mkutano huo ulisimama kwa dakika tano hadi mwananchi huyo alipoondolewa kwenye mkutano huo.