Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chadema yaendelea kujifungia, maazimio kutolewa

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu

Muktasari:

  • Miongoni mwa mambo yanayojadiliwa ni hali ya siasa nchini nchini operesheni za chama na kamati maalum ya chama Zanzibar.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema bado kinaendelea na vikao vyake vya kamati kuu kikijadili hali ya siasa nchini nchini operesheni za chama na kamati maalum ya chama Zanzibar.

Kauli hiyo inakuja ikiwa ni siku ya pili tangu kamati hiyo ijifungie kwa kikao cha kawaida cha robo ya pili ya mwaka 2023/24.

Kikao hicho kimefanyika zikiwa zimepita wiki tangu chama hicho kilipomaliza ziara zake za mikutano ya hadhara katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mara na baadhi ya wilaya za Mkoa wa Arusha.

Chama hicho pia kimejifungia ikiwa imepita wiki moja tangu kiliposusia mkutano wa Baraza la Vyama vya siasa uliofunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Septemba 11, licha ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Zanzibar), Said Issa Mohammed kuhudhuria kupitia kamati iliyoundwa na Rais Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Septemba 22, 2023 na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alipotoa taarifa fupi ya kikao hicho.

"Ni kikao cha robo ya pili ya mwaka, ni cha kawaida na mara nyingi tunajadili hali ya siasa nchini.

"Tunapokea ripoti ya taarifa za operesheni za chama na kamati maalum ya chama Zanzibar ni kikao cha kawaida cha siku mbili na kinahitimishwa leo," amesema.

Kuhusu maazimio, Mwalimu amesema ni mapema kuyajua na kwa kuwa kikao kinaendelea utaratibu utaandaliwa kwa ajili ya kueleza yatakayoazimiwa kwa umma.

Wingi wa ajenda, kulingana na Mwalimu ndiyo sababu ya kikao hicho kufanyika kwa siku mbili ingawa ni kawaida.

"Ni kikao cha kawaida kabisa, na baada ya kutoka hapa tutawaita kuzungumza na ninyi kuwaeleza ni kitu gani tumekiazimia," amewaleza waandishi wa habari.