CCM yazindua kampeni za ubunge Amani

Muktasari:

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kampuni za uchaguzi mdogo wa ubunge wa Aman, visiwani Zanzibar utakaofanyika Desemba 17, 2022.

Unguja. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kampuni za uchaguzi mdogo wa ubunge wa Aman, visiwani Zanzibar utakaofanyika Desemba 17, 2022.

Kampeni hizo zimezinduliwa leo Alhamisi, Desemba 1, 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka pamoja na mambo mengine, amemnadi mgombea wa chama hicho, Abdul Yussuf Maalim.

Katika uzinduzi huo, Shaka amewataka wananchi wa jimbo hilo kuchagua mgombea iliyemsimamisha kwa kuwa CCM ndiye mwenye uwezo wa kuendeleza kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Amesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dh Hussein Ali Mwinyi amefanya kazi kubwa na nzuri, hivyo anastahili kupewa viongozi watokanao na CCM ili kuendeleza Kasi hiyo.

Aidha, amesema kazi ya kuleta maendeleo hususan katika jimbo hilo haiwezi kuletwa na kila mtu, hivyo kuna kuna umuhimu mkubwa wa kumchagua mgombea aliyesimamishwa na CCM.

“Kazi ya kuleta maendeleo ya nchi hii hapewi kila mtu, kazi ya kuleta maendeleo jimbo la Amani sio kila mmoja anaweza kuleta maendeleo, wapi wenye uwezo wa kuleta propaganda kwenye jimo la Amani.”

“Lakini wapo wenye uwezo wa kuleta maendeleo wana amani mkasema kweli haya ni maendeleo ambayo tunayahitajia, ndiyo maana tukasema Abdul songa mbele nenda ukapeperushe bendera ya Chama Cha Mapinduzi,” amesema Shaka

"Ushindi wa CCM katika Jimbo la Amani ni kama kufa na kupona, tutashinda kwa haki, tutashinda kwa amani, lakini tutashinda tukiwa wamoja na tumeshikamana," amesisitiza

Amesema kazi nzuri iliyofanywa na Rais Samia katika kipindi cha miaka miwili ni kubwa hivyo anastahili kupongezwa na juungwa mkono ikiwamo kumchagulia wagonbea watokanao na CCM.

"Ndani ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Dk Mwinyi mtu apende asipende, afurahi asifurahi Dk Mwinyi ameupiga mwingi (amefanya vizuri kuleta maendeleo).”

Shaka amesema, “mabadiliko tunayoyashuhudia Zanzibar...lazima tukubali matarajio ya wazanzibari kwa Dk Mwinyi ni makubwa zaidi."

Kwa upande wake mgombea huyo, amesema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge amejipanga kuendeleza kasi ya maendeleo kwa kushirikiana na Rais Mwinyi na viongozi wengine wa chama, serikali na wananchi kwa ujumla.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Desemba 17, mwaka huu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Maalim Mussa.