Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa nini umfiche mwenza wako kipato?

Muktasari:

  • Kama siri inalenga kujenga na kuimarisha ndoa, inafaa na kuswihi. Kama siri husika ni ya kubomoa ndoa, basi iepukwe mara moja.

Canada. Hakuna kitu kizuri na chenye faida na furaha kwa wanandoa kama kutofichana mambo au siri.

 Hapa tutaongelea athari na madhara ya kufichana kipato au kila mwanandoa kuwa na chake badala ya chetu. Wanandoa wanapokuwa wawazi, licha ya kuwapa kuaminika na kujiamini, huwasaidia pale wanapokumbwa na misukosuko ya kifedha au kiuchumi kama vile kufilisika, kuachishwa kazi, kuugua, na mengine kama hayo. 

Faida nyingine ya kutoficha kipato ni kutosumbuliwa kwa kudaiwa matumizi ambayo mhusika hana uwezo nayo. Mbali na hilo, pia, hujenga kuaminiana na kushirikiana katika dhiki na raha.

Faida nyingine ya kutokuwa na siri ni ule uhuru katika maisha ukiachia mbali kutojiruhusu kuujengea moyo wako shinikizo litokanalo na kutunza siri au uwezekano wa kufichuliwa siri. 

Kimsingi, siri ni kama mgando kwenye moyo  wa mwenye kuiweka. Au tuseme ni moto unaounguza taratibu wenye kusababisha maumivu makali na makubwa yasiyotabirika wala kuisha. 

Siri ni mateso kwa mwenye kuitunza hasa siri yenyewe inapokuwa haina ulazima. Mwenye kuficha siri hana uhuru wala amani moyoni. Mwenye kutunza siri inayoweza kuivunja ndoa yake hana tofauti na mgonjwa wa saratani. 

Haiponi na mwisho wake ni maangamizi na misiba kwa wanandoa na familia zao. Kimsingi, mwenye kuwa na siri ana mzigo mkubwa tena unaoumiza moyo wake kila siku mbali na kumgharimu fedha, furaha, hata uhai wakati mwingine.

Kitu kingine kinachoweza kutoa funzo na mwanga juu ya siri ni ule ukweli kuwa duniani hakuna siri tena siri ya watu wawili au zaidi. 

Ipo siku, kama harufu, inzi mmoja ataifichua na kuwaumbua na kuwaumiza wenye siri husika. Hii ni kutokana na ukweli kuwa binadamu hatutabiriki. Wewe unaweza kutunza siri yako. Je, mwenzako au wenzako wanaweza? Kawaida, siri huvuja pale mmoja wa watunza siri anapofurahi au kuchaganyikiwa akaitoboa kwa mwingine adhaniye naye ataitunza kama yeye asijue bindamu hatutabiriki na tunabadilika. Kama serikali yenye maguvu na vyombo vyote vya usalama inatunza siri za uhai na utendaji wake, wanandoa ni nani wasifanye hivyo? 

Kama Mungu ametunza siri kama vile ya uumbaji na kifo, sisi ni nani tuanike siri zetu hadharani. Kwa faida gani na ya nani wakati tunajua hatari na madhara ya kufanya hivyo. Tia maanani. Dawa ya siri ni kutokuwa na siri.


Turejee kwenye somo

Turejee kwenye kipato. Mfano, utakuta baba au mama anajali kazi yake kuliko hata ndoa! Tunakwenda wapi huko kusiko na maana wala mwelekeo? 

Busara haachi kuhoji hata akiitwa mkale na aliyepitwa na wakati. Ajabu, huyu anayejali kazi na kuvunja ndoa yake, akimaliza, hujikuta kazi haimtoshelezi kiasi cha kuanza kutafuta ndoa,huku Kwa hata watu wazima wakihaha  kuwaandama hata kuwatumia vijana wa umri wa watoto wao. Je huku si kudhalilika au kujidhalilisha?

Nani alijua kuwa ndoa inahitaji karatasi badala ya mapenzi na uaminifu? Tumeona makasisi wakizini hadi kufikishwa mahakamani. Wengine wamenajisi hadi kuuawa kwenye uchafu wao. 

Wengine wanaongozwa na mashoga. Je,, hawa na wauaji wana tofauti? Lakini bado wanatunza siri hii ambayo baadaye hufichuka na kuwaumbua na kuwaumiza. Maana, muuaji siyo auwaye mwili bali hata auawaye roho. Auwaye roho ni muuaji mbaya kuliko auawaye mwili. Mwili huoza. Nani anajua majaliwa ya roho iliyouawa na wale iliowaamini wakati hawaaminiki? 

Nani anajali wala kujiuliza swali kama hili? Kisu na mnafiki heri kisu maana waweza kukitahadhari. Heri mlevi umuonaye mtaani kila siku kuliko mnafiki aliyejificha kwenye utawa au madaraka akidhani ni siri. Tusemayo siyo mapya, jipya ni kuyasema na kuyaandika.

Tumalizie kwa kushauri na kusisitiza kuwa hakuna faida ya kuwa na siri kwa wanandoa ingawa ni vizuri kutunza siri za ndoa yao huku wakiepuka kuwa na siri nje ya ndoa yao. 

Siri ni mbaya na nzuri kutegemea na hiyo siri ni juu ya nini, inawahusisha nani na kwa faida gani na ya nani. 

Kama siri inalenga kujenga na kuimarisha ndoa, inafaa na kuswihi. Kama siri husika ni ya kubomoa ndoa, basi iepukwe mara moja.

Mwisho, katika ndoa hakuna kazi wala mali yangu au yake bali yetu hata kama mna kazi, mali, na majukumu tofauti.