Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kama wakwezo wanga, wazazi wako nao wanga

Muktasari:

  • Watu wanga wapo kweli au ni matokeo ya ukosefu wa sababu za msingi za kuelekea na kutatua tatizo?

Canada. Ni mara ngapi umesikia malalamiko na tuhuma za uchawi katika baadhi ya familia za wanandoa wawe wanaokuhusu au kutokuhusu?

Huwa unajisikiaje na kuelewaje? Si jambo jipya kusikia fulani akilalamika kuwa wakwe zake ni wanga. Mara nyingi, malalamiko haya hutolewa na wakamwana wanaposhindwa kuelewana na mama wakwe hata baba wake zao.

Je, malalamiko haya yana ukweli au ni ya kupuuza? Je, ni ya kuchukulia kwa umakini? Wanga upo kweli au ni matokeo ya ukosefu wa sababu za msingi za kuelekea na kutatua tatizo? Hivi  yakikuta wewe au ndugu hata rafiki, utachukua hatua gani mujarabu?

Katika tuhuma za ‘wanga’,  watuhumiwa wengi, au tuseme waathirika, ni mama wakwe. Baba wakwe, mara nyingi, huingizwa kwa kuunganishwa na wake zao ndipo wawe ‘wanga.’

Hata kwenye tuhuma za uchawi nje ya wanandoa, mara nyingi, wengi ni wanawake na si wanaume. Tunadhani hii ni kutokana na ukaribu wa wakazamwana na mama wakwe zao.

Pia, inaweza kutokana na ukweli kuwa, mara nyingi, watoto huwa karibu na mama zao kuliko baba zao japo si wote.

Sababu nyingine inaweza kuwa mfumo dume unaowadhalilisha wanawake na kuwatwisha kila lawama na mizigo ya kijamii.

Hata hivyo, wakati tukidurusu na kutafakari dhana nzima ya wanga, tujiulize maswali kadhaa:

 Je, kweli wakwe wanaotuhumiwa ni wanga kweli au mwanga ni yule anayewatuhumu? Wanga unaweza kuthibitishwa kisayansi? Kisheria, tunajua wazi, wanga hauwezi kuthibitishwa. Ni matokeo ya ujinga na imani za ovyo. Ni kweli wanga upo na wahusika wanaufanya? Ili iweje?

Tukiangalia tuhuma za wanga dhidi ya wake, kuna baadhi ya maswali ya ziada ya kujiuliza; ilikuwaje, kama kweli ni wanga, waliweza kumlea huyo mumeo hadi akakua na kukuoa wasimuwangie na hata kumua? Angekuwa mama yako au wazazi wako wote ndiyo wanaotuhumiwa wanga na mwenzi wako ungefanya nini?


Nini kifanyike?

Katika kudurusu na kuchunguza dhana hizi za kijinga zitokanazo na chuki na ukosefu wa umakini katika kuendea matatizo, tunapendekeza hatua zifuatazo kuchukuliwa ili kuepusha kusambaratisha ndoa hata jamii.

Mosi, ni vizuri kwa wanandoa kujielimisha juu ya dhana nzima ya uwanga na sababu za kuwepo kwake ziwe za kweli, uongo, chuki, hata kisayansi.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa dhana hizi zipo. Hivyo, haziwezi kufumbiwa macho hasa ikizingatiwa kuwa madhara yake huwa mabaya na makubwa.

Pili, wanandoa waepuke chuki na dhana potofu ambazo nazo huchangia sana uwepo wa dhana hizi mbovu. Baya zaidi, wahusika wanaposhindwa kutumia akili kutatua tatizo ambalo laweza kwa chuki binafsi, uchoyo, hata umaskini, hupanua wigo wa tatizo kwa kuhusisha wapiga ramli, wachungaji, na hata mashoga ambao huongeza hatari kwa wanandoa na familia zao. 

Kwa mfano, mwathirika anaweza kwenda kwa mganga wa kienyeji au mchungaji ili kuaguliwa, kuzindikwa, hata kuombewa bila kujua kuwa hao anaowapelekea matatizo yake, wakati mwingine, wanakuwa na matatizo makubwa kuliko yake.

Tatu, jamii inapaswa kuachana na unyanyasaji wa kijinsia ambapo waathirika wakubwa huwa ni wanawake zaidi ya wanaume.

Katika utafiti aliofanya Dk Philippa Carter, mwaka 2023, aligundua kuwa huko Marekani na Uingereza, kulikuwa na matukio ya  tuhuma za uchawi. Watuhumiwa wote walikuwa 802 kulingana na rekodi za mpiga ramli maarufu wa Uingereza Richard Nappier (1559-1 April 1634) na kugundua kuwa kati ya watuhumiwa hao, 500 walikuwa wanawake na wanaume 232 ambapo malalamiko 70 hayakuwa yameorodheshwa.

Katika kitabu chake  Malleus Malleficarum (2023), mwandishi Heinrich Kramer alibaini kuwa, kutokana na wanawake kuwa hadhi ya chini ikilinganishwa na wanaume, ni chanzo kikubwa cha kutuhumiwa uchawi.

Nne, tunashauri kuwa kabla ya kuwashutumu wengine, jiweke kwenye viatu vyao na kufikiri nje ya boksi. Je utajisikiaje kama wifi yako atawatuhumu wazazi wako kuwa wanga wakati unajua si wanga bali chuki na hila tu?

Utakapozeeka, likikutokea hili, utajisikiaje? Japo hili hulioni, kwa namna ulivyo mnyama, Mungu lazima atakulipa, kwani malipo ni hapa hapa.

Usishangae yakakukuta haya unayowafanyia wenzako tena bila sababu yoyote bali ujinga, roho mbaya, uroho, na kushindwa kufikiri sawa sawa.