Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisasi cha mtoto kwa mzazi ni matokeo ya maumivu uliyompa

Muktasari:

Katika jamii nyingi, mzazi huonekana kama kielelezo cha ulinzi, upendo na mwongozo kwa mtoto. Hata hivyo, si watoto wote wanaokulia katika mazingira yenye upendo na ulinzi wa kweli.

Wazazi wanapaswa kutambua kuwa athari za malezi mabaya hazikomei utotoni, bali huenda zikatawala maisha ya mtoto hata akiwa mtu mzima.

Kupitia upendo, uelewa na mawasiliano, tunaweza kuvunja mzunguko wa mateso na kujenga kizazi chenye afya ya mwili na akili.

Siku njema huonekana tangu asubuhi, Waswahili ndivyo wasemavyo, msemo ambao pi ulianza kutumika tangu enzi za mababu na mabibi zetu.

Hivyo, vivyo hivyo, mzazi bora hujengwa kwa uamuzi bora tangu angali mdogo.

Katika jamii nyingi, mzazi huonekana kama kielelezo cha ulinzi, upendo na mwongozo kwa mtoto.

Hata hivyo, si watoto wote wanaokulia katika mazingira yenye upendo na ulinzi wa kweli. Wapo watoto wanaolelewa kwa mateso ya kimwili, ya kihisia na ya kisaikolojia, ambayo kwa bahati mbaya huacha makovu ya muda mrefu katika maisha yao.

Matokeo ya makovu haya huweza kujitokeza baadaye kwa njia ya kisasi cha kimya au dhahiri dhidi ya wazazi wao, ama kupitia tabia, maneno, au matendo ambayo huumiza familia nzima na hata jamii.

Wataalamu wa saikolojia niliofanya nao mazungumzo kwa nyakati tofauti, waliniambia kuna aina ya visasi ambavyo watoto huweza kuwalipiza wazazi wao ambao waliwatendea ndivyo sivyo walipokuwa wadogo.

Miongoni mwavyo nia kutowajali wazazi wao wanapofikia umri wa uzee. Wanasema kisasi hiki hutokea pale mtoto aliyeteswa au kutelekezwa anapofikia umri wa utu uzima,  anakataa kuwatunza wazazi wake wanapohitaji msaada wake.

Huwa hana huruma wala hisia zozote za kuwajali, akiamini walistahili adhabu hiyo kwa kuwa walimtesa awali.

Lakini watoto wengine huamua kukata kabisa mawasiliano na familia zao. Hawapigi simu, hawatembelei nyumbanina hata kwenye matukio ya familia kama vifo au harusi, hawaonekani.

Na wao mara zote huona kujitenga ni njia ya kulipa kisasi na kulinda afya yake ya akili.

Wengine huchagua kuwasuta hadharani wazazi wao kupitia mitandao ya kijamii, mahojiano au hata katika kazi zao za sanaa kama uandishi au muziki.

Hili ni jaribio la kuonyesha ulimwengu kuwa wao waliathiriwa na wazazi wasio na huruma.

Baadhi ya watoto huelekeza maumivu yao kwa jamii kwa kutenda matendo ya hatari ikiwamo ukatili kwa wengine na baadhi huamua kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Wengine hujikuta wakirudia historia kwa watoto wao kwa sababu ya hasira waliyonayo kwa wazazi wao.

Huwa wamejeruhiwa kiasi cha kutoweza kumpenda au kumlea mtoto wao kwa njia bora, hivyo kuendeleza mzunguko wa mateso kizazi hadi kizazi.

Ila kuna baadhi ya watu wanaweza kujiuliza zaidi kwamba chanzo ha kisasi hicho hasa ni nini na ikizingatiwa kuwa huyu ni mtoto tu ambaye hapaswi kuonyesha jeuri kwa wazazi wake.

Kisaikolojia, mtoto anayekulia katika mazingira ya unyanyasaji hupoteza imani kwa mtu yeyote, hasa wale waliopaswa kumlinda ambao ni pamoja na wazazi wake.

Maumivu ya kihisia yanapokusanywa bila kufanyiwa kazi, humjengea chuki ya muda mrefu.

Akikua, mtoto huyo hujenga uwezo wa kujilinda na kujitenga na kisasi huchukuliwa kama njia ya kurejesha heshima au kudhibiti maumivu ya zamani aliyopitia.

Sasa ili mzazi ujiepushe na madhira haya, unapaswa kusisi kwenye malezi ya upendo na uelewa.

Wazazi wanapaswa kuelewa kuwa upendo haumaanishi kulea kwa ulegevu, bali ni kutoa nidhamu kwa heshima na mawasiliano ya wazi.

Kwa sababu mtoto anapohisi anapendwa na kusikilizwa, hujenga msingi wa kujiamini na heshima kwa wazazi wake.

Lakini pia mazungumzo ya mara kwa mara, kuelewa changamoto wanazopitia na kuepuka dharau dhidi ya hisia zao, ni njia muhimu ya kuzuia majeraha ya kihisia. Ila tukumbuke kuwa wazazi ni binadamu.

Kuomba msamaha kwa mtoto ni hatua ya kishujaa inayojenga daraja la uaminifu. Mtoto akijua mzazi wake anaweza kukiri makosa, hupunguza maumivu aliyobeba.

Ikiwa mzazi anakabiliwa na hasira, msongo wa mawazo au historia ya unyanyasaji, ni muhimu kutafuta msaada wa kitaalamu ili asiendelee kuumiza watoto wake. Vilevile, mtoto aliyepitia unyanyasaji anapaswa kusaidiwa mapema.