Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo haya kukujenga kuwa mwanafunzi bora shuleni

Muktasari:

  • Mwanafunzi bora anajua kipaji chake.Unaweza kufanikiwa katika maisha kupitia elimu au kipaji chako.Kipaji kwa sasa kina nafasi kubwa sana kikiambatana na elimu.

Kuna msemo usemao: ‘’Walimu watakufungulia milango ila kuingia ndani ni hiari yako."

Walimu walikutengenezea njia ya kuendelea tangu ulipokuwa shule ya msingi.Kuendelea kuwa bora ni hiari yako siyo tena jukumu la walimu japo wana nafasi hiyo siku zote.

Tutazame mwanafunzi bora ana sifa gani maana wanafunzi nao wana madaraja yao. Mosi, ni mwanafunzi mtafuta taarifa.

Mwanafunzi yeyote ambaye kwa sababu moja ama nyingine anaweza kukosa vipindi kadhaa au kutofika shule kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake, anapofika tu shule jambo la kwanza huwa anauliza wenzake yake yaliyojili shule.

Huanza na vipindi vilivyofundishwa na matangazo yanayomhusu yaliyotolewa na walimu kwa muda ambao yeye hakuwapo shule.Mwanafunzi mwenye sifa hizi huwa ni mwanafunzi bora anayejua anafanya nini shule.

Pili, ana malengo. Mwanafunzi bora ana malengo thabiti na anajua kwanini yupo shule na anafanya nini shuleni? Jambo hili la malengo nilishalizungumza katika makala zilizopita.

Ninachokusudia hapa ni kujua kwanini mwanafunzi yupo shule na anatakiwa kufanya nini akiwa shule na baada ya kuhitimu elimu yake anatakiwa kutoka na nini au atapata nini. Hayo ndiyo malengo.

Tatu, kujitambua. Ili mwanafunzi aonekane kuwa anajitambua ni lazima awe na utambuzi wa kiroho (dini), kimwili, kitaaluma, kihisia na kijamii (kuijua jamii yake na kumpa kila mtu stahiki yake katika jamii.

Nne, mwanafunzi bora ana nidhamu muda wote anapokuwa shule, kiasi kwamba walimu wanajivunia kuwa naye na kumtolea mfano kwa wanafunzi wengine.

Tano, ni mwanafunzi asiyejitenga na wengine kwa kwa kujiona kuwa yeye anaweza sana au yeye ni wa pekee au ni bora zaidi ya wengine. Na hata kama sifa hizo atakuwa nazo bado atapenda kuonekana wa kawaida siku zote mbele ya wengine.

Sita, mwanafunzi bora anajua namna ya kutunza muda katika shughuli zote zinazomhusu kitaaluma ikiwemo shughuli zote za darasani na za nje ya darasa.

Mafanikio yamefichwa katika muda na watu wote waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali, ukiwauliza siri ya mafanikio yao, hawataacha kutaja matumizi mazuri ya muda.

Saba, mwanafunzi bora anajua kipaji chake.Unaweza kufanikiwa katika maisha kupitia elimu au kipaji chako.Kipaji kwa sasa kina nafasi kubwa sana kikiambatana na elimu.

Unaweza kufanya makubwa kwa dunia ya sasa kupitia kipaji ila kipaji kikiambatana na elimu unafika kule ambako wengine hawakuwahi kufikiri kuwa unaweza kufika.

Unaweza kujua kipaji chako kwa kuuliza watu wa karibu yako kuhusu uwezo wako, kushiriki na kufanya kila kitu ambacho unadhani unaweza au kupenda kama vile kucheza mpira, mashindano ya uandishi na mengine mengi.

Mwisho muulize mzazi wako na hasa mama kwa kuwa muda mwingi yeye ndiye aliyekuwa karibu na wewe katika hatua zako zote za ukuaji. Anakujua na ndiye anayeweza kukutajia vipaji vyako.