Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkuchika: Tanzania imepiga hatua vita dhidi ya rushwa

Muktasari:

Mkutano wa mwaka wa Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika (AUABC) umeanza leo Oktoba 2, 2018, unahudhuriwa na wakuu wa taasisi za kupambana na rushwa barani Afrika wenye lengo la kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi.

Arusha. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema Serikali imepiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa hatua iliyoongeza mapato kutoka Sh800 bilioni kwa mwezi hadi Sh1.2 trilioni.

Akifungua mkutano wa mwaka wa Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika (AUABC) leo Oktoba 2, 2018 yenye makao yake jijini Arusha amesema licha ya mafanikio hayo bado vita dhidi ya rushwa inaendelea kwani mbinu zimekuwa zikibadilika kila wakati.

Amesema katika nchi za Afrika Mashariki Tanzania ipo nafasi ya pili ikitanguliwa na nchi ya Rwanda kwa mafanikio ya kupambana na rushwa na katika kipindi kifupi kijacho itakua ya kwanza.

"Rais John Magufuli amedhihirisha wazi vita yake dhidi ya vitendo vya rushwa hatua ambayo imeongeza mapato na kuwa na uwezo wa kununua ndege na kutekeleza miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa," amesema Mkuchika

Amesema kwa muda mrefu mataifa makubwa yamenufaika kupitia rasilimali za Afrika hatua ambayo Serikali ya awamu ya tano iliamua kupiga marufuku usafirishaji wa Makinikia ili madini yawanufaishe wananchi.

Mbunge kutoka nchini Mauritius, George Lesjongard amesema rushwa imekuwa chanzo cha machafuko, uvunjifu wa amani na utawala usiozingatia sheria katika maeneo mbalimbali Afrika.

Amesema ili kukabiliana nayo ipasavyo mifumo ya kisheria na taasisi za kupambana na rushwa hazina budi kujengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yake ipasavyo sanjari na kuongeza uwajibikaji na uwazi katika taasisi za serikali.

Ameongeza kumekuwa na changamoto ya kurejesha fedha zinatoroshwa nje ya bara la Afrika kutokana na mkwamo wa kisheria kwenye mabenki zilikofichwa fedha hizo.

Mwenyekiti wa bodi ya AUABC, Begoto Miarom amesema kumekuwa na mafanikio katika kupambana na rushwa kubwa licha ya taasisi hiyo kuwa changa miongoni mwa taasisi za Umoja wa Afrika.