Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkuchika awataka Wanaccm kuirudisha Mtwara sehemu yake

Mtwara. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Kazi maalum ambaye pia ni Mbunge wa Newala Mjini (CCM), Kapteni George Mkuchika amewataka wanachama wa chama hicho mkoani humo kuurudisha mkoa nafasi ya juu katika chama.

Mkuchika amesema katika uchaguzi wa mwaka 2005 mkoa ulishika nafasi ya tatu kuipenda CCM lakini mwaka 2020 uliporomoka hadi kufika nafasi ya 16.

"Nawaomba leo chagueni timu itakayorudisha Mtwara kwenye tatu bora au hata namba moja na yenye uchungu na mkoa wetu, uwezo tunao kama mkoa tujiulize," amesema Mkuchika

Mkuchika amesema hayo katika mkutano wa uchaguzi wa Mwenyekiti na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa unaofanyika leo Jumatatu, Novemba 21, 2022 wilayani Masasi.

Mwenyekiti CCM mkoa anayemaliza muda wake, Yusuf Nannila amesema chama kinarudi nyuma mkoani hapa kwa sababu viongozi wanafanya kazi za watu.

Amesema kwa kipindi chote alichoshikilia nafasi hiyo amegundua kuwa  moja ya athari kubwa ni watu kufanya kaz za watu badala ya Chama.

"Makundi acheni kufanya kazi za watu mkafanye kazi za chama mliochaguliwa na mtakaochagulowa hapa twendeni tukafanye kazi za chama" amesema Nannila.

Msimamizi wa uchaguzi huu ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala ameomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wajumbe ili uchaguzi uishe mapema kwa haki.