Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Macha ataka waajiri wawaruhusu wafanyakazi kushiriki Mei Mosi

Muktasari:

  • Sherehe hizi si tu haki yao, bali ni njia ya kuimarisha mshikamano, mahusiano na kuongeza morali ya kazi.

Shinyanga. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha amezindua rasmi wiki ya maadhimisho kuelekea Siku ya Wafanyakazi Duniani itakayofanyika Mei mosi, 2025, huku akitoa wito kwa waajiri wote kuwaruhusu wafanyakazi wao kushiriki kikamilifu katika shughuli hizo.

Akizungumza na wananchi leo Jumamosi, Aprili 26, 2025, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo  uliofanyika katika uwanja wa Kambarage uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga, amesema, "Waajiri wanapaswa kuelewa kuwa ushiriki wa wafanyakazi katika sherehe hizi si tu haki yao, bali ni njia ya kuimarisha mshikamano, uhusiano kazini na kuongeza morali ya kazi.

"Wiki ya wafanyakazi ni fursa ya kipekee kwao kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo huduma za afya na elimu, ambazo zinalenga kunufaisha wananchi moja kwa moja."

Aidha, Macha amesisitiza umuhimu wa uhusiano mzuri kati ya waajiri na wafanyakazi, akibainisha kuwa ushirikiano huo ni kichocheo kikubwa cha kuongeza tija na ufanisi sehemu ya kazi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) Mkoa wa Shinyanga, Yohana Maremi amesema kabla ya uzinduzi huo wanachama wamejitolea kufanya usafi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

"Kama sehemu ya kuadhimisha wiki ya wafanyakazi, jitihada za kusafisha zimeboresha mazingira ya utoaji huduma hospitalini kama uwajibikaji wa kijamii kwa watumishi," amesema Maremi.

Mmoja wa wafanyakazi kutoka sekta binafsi, Fatuma Abdallah amesema maadhimisho hayo yanajenga uhusiano mzuri kwa wafanyakazi wa sehemu tofauti.

"Maadhimisho haya yanakutanisha wafanyakazi wasiofahamiana na kujenga ushirikiano mzuri katika kulijenga taifa moja," amesema Fatuma.

Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu "Uchaguzi Mkuu 2025, tuletee viongozi wanaojali haki na maslahi ya wafanyakazi, tushiriki sote."