Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Biteko ateta na viongozi CPC

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  dk Doto Biteko akipokea  Kitabu maalum cha "The Governance of China" kutoka kwa Mjumbe wa Kamati na Mkurugenzi Mkuu wa Bureau I, Idara ya Oganizesheni ya Kamati Kuu ya Chama cha CPC,  Ndugu Mao Dingzhi ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Novemba28 , 2023

Muktasari:

  • Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amefanya mazungumzo na Uongozi wa juu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) huku akieleza kuwa Watanzania wanahitaji kujengewa uwezo wa utawala na teknolojia.

Dar es Salaam. Wakati China ikitajwa ni miongoni mwa mataifa yaliyopiga hatua zaidi kwenye teknolojia, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amewaomba ushirikiano wa Tanzania na China ujikite kwenye kukuza masuala ya utawala na teknolojia. Kwa mujibu ya Global Finance 2023, China ni nchi ya 38 kwa kuwa na teknolojia ya hali ya juu duniani.

Waziri Biteko ametoa ombi hilo leo, Jumanne Novemba 28, 2023 jijini hapa, alipokutana na viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ukiongozwa na Mao Dingzhi  ambaye ni Mjumbe wa Kamati na Mkurugenzi Mkuu wa Bureau I, ambayo ni Idara ya Oganaizesheni ya Kamati Kuu ya CPC, akiwa ameambatana na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian.

Dk Biteko, amesema ukuaji wa teknolojia duniani unahitaji watalaamu waliobobea hivyo na China wamefanikiwa kwenye eneo hilo hivyo anaamini ushirikiano wao utasaidia Tanzania kufikia malengo iliyojiwekea katika kukuza teknolojia na utawala.


Katika mazungumzo hayo Dingzhi ampongeza Dk Biteko kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na ameishukuru Tanzania kuiunga mkono Serikali ya China kwenye majukwaa mbalimbali ya kimataifa.

Dingzhi amesema CPC na Chama cha Mapinduzi (CCM) vimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu tangu enzi ya waasisi wa vyama hivyo ambao ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tse Tung na kuongeza kuwa ushirikiano huo unaendelezwa na vyama hivyo hadi sasa.

Amepongeza jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuwezeshaTanzania kuwa nchi ya amani, yenye uhuru wa kutoa maoni, uzalendo na kuheshimu utu wa wananchi wake na kuahidi kuendeleza ushirikiano kwenye nyanja za uchumi wa kidijitali, masuala ya kijamii, utamaduni pamoja na elimu.