Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili wahofiwa kufariki ajalini Same

Same. Watu wawili wanahofiwa kufa katika ajali iliyohusisha basi la Kilimanjaro Express na gari dogo iliyotokea wilayani Same.

Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Kijomu, kilichopo kata ya Hedaru. Basi hilo lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam liligongana na gari dogo walimokuwa watu hao wanaodhaniwa kuwa wanandoa.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Mtendaji wa kijiji hicho aliyekuwa eneo la ajali, Veran Mtenga amesema imetokea leo Juni 23, 2023 saa 12 asubuhi.

"Baada ya kupata taarifa saa 12 asubuhi nilifika eneo la tukio, nilikuta basi la Kilimanjaro na gari dogo ambalo lilikuwa  limeharibika, kwenye  gari dogo  kulikuwa na  watu miwili, mwanamke na mwanaume," amesema.

Jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilmanjaro, Simon Maigwa kujua chanzo cha ajali hiyo hazikuzaa matunda licha ya kupigiwa simu na kutaka atumiwe ujumbe wa SMS kwa kuwa yupo kwenye kikao.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.