Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu waliofariki kwa maporomoko ya udogo wazikwa

Majeneza yenye miili ya watu watatu wakiwemo wawili wa familia moja yakiwa katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Fukeni.



Muktasari:

  • Maziko yamefanyika leo Mei 10, 2025 katika vijiji vya Tema na Korini vilivyopo Kata ya Mbokomu, wilayani Moshi.

Moshi. Miili ya watu watatu wakiwamo wawili wa familia moja, waliofariki dunia baada ya nyumba zao kuporomokewa na udongo kutokana na mvua zinazonyesha mkoani Kilimanjaro wamezikwa.

Maziko yamefanyika leo Mei 10, 2025 katika vijiji vya Tema na Korini vilivyopo Kata ya Mbokomu. Tukio hilo lilitokea usiku wa Mei 6, 2025.

Miili iliagwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Fukeni wilayani Moshi.

Ester Mlinga na mwanaye Emmanuel Mlinga wamezikwa katika Kijiji cha Korini, huku mwili wa Zaina Langstone (65) ukizikwa katika Kijiji cha Tema.

Mchungaji Kennedy Kisanga, katika ibada ya mazishi amesema kifo ni fumbo na kila mtu ana namna yake ya kuondoka duniani, hivyo kila mmoja akae karibu na Mungu wakati wote kwa kutenda yaliyo mema.

Baadhi waombolezaji wakati wa ibada ya mazishi ya watu watatu wakiwemo wawili wa familia moja, iliyofanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Usharika wa Fukeni. Picha na Omben Daniel

Ametoa pole kwa familia hizo na kuwataka waombolezaji kuishi kwa upendo na kila mmoja na kuwa na hofu ya Mungu.

"Kufiwa si jambo rahisi, nitoe pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, najua kila mtu ataondoka kwa namna yake hapa duniani, amini maisha yetu yapo mikononi mwa Mungu, tujiandae kila wakati hapa dunia. Hawa wenzetu hawakuugua lakini ndio hivyo, Mungu amewapenda waondoke kwa namna hiyo," amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava ametoa pole kwa familia akisema Serikali ipo pamoja nao kwa kila hatua.

"Tumpe pole baba aliyepoteza mke na mtoto na wengine watatu ambao wapo hospitali wanaendelea na matibabu. Tumewatembelea hospitalini wanaendelea vizuri," amesema.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na familia wataendelea kuratibu shughuli na kusimamia mazishi.

Katika historia ya marehemu hao, Wisman Mlinga ambaye amepoteza mama na mdogo wake, amesema ndugu zake walifikwa na umauti wakiwa wamelala usiku wa manane.

Zaina amefariki dunia kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yake.