Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu wafariki kwa kuangukiwa na nyumba Moshi

Wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro wakiondoa magogo katikati ya Barabara Kuu ya Dar es salaam – Moshi - Arusha, eneo la Kiboriloni Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro leo Jumanne 6, 2025.

Muktasari:

  • Watu watatu, wakiwemo wawili wa familia moja, wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Mei 6, 2025, baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuangushwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro.

Moshi. Watu watatu, wakiwemo wawili wa familia moja, wamefariki dunia katika Kata ya Mbokomu, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, baada ya kuangukiwa na nyumba yao kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, Mei 6, 2025, ambapo waathirika walikuwa wamelala ndani ya nyumba hiyo wakati janga hilo lilipotokea.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kueleza kuwa shughuli za kuondoa miili ya marehemu zinaendelea kwa ajili ya maandalizi ya maziko.

“Ni kweli, kuna watu watatu wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na nyumba wakiwa wamelala usiku wa kuamkia leo, katika Kata ya Mbokomu,” amesema DC Mnzava.

Aidha, DC Mnzava amesema kuwa katika hatua nyingine, shughuli za kusafisha barabara kuu ya Moshi–Arusha–Dar es Salaam, katika eneo la Kiboriloni, Manispaa ya Moshi, zinaendelea.

Barabara hiyo ilikuwa imezibwa na magogo, miti na matope kutokana na mafuriko, lakini juhudi za kuirejesha katika hali ya kawaida zinaendelea kwa kasi.

“Muda si mrefu magari yataanza kupita baada ya kuondoa vizuizi vilivyosababishwa na mafuriko,” ameongeza.