Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanakwaya sita wafariki dunia, 75 wajeruhiwa ajali mbili tofauti Same

Muktasari:

  • Ajali hiyo imetokea katika Barabara ya Bangalala ambapo gari aina ya Coaster lililowabeba wanakwaya hao lilipoteza mwelekeo na kupinduka na kusababisha vifo vya wanakwaya sita na majeruhi 23

Same. Watu saba wakiwamo wanakwaya sita wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Chome, Usharika wa Mmeni, wamefariki dunia papo hapo huku wengine 23 wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kupinduka katika Milima ya Pare, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni ameithibitishia Mwananchi kutokea kwa ajali hiyo leo Jumapili Machi 30, 2025, saa nne asubuhi katika Barabara ya Bangalala. Mkuu huyo wa wilaya amesema wanakwaya hao walikuwa wakisafiri kutoka Chome kuelekea Vudee ndani ya wilaya hiyo.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu katika mfumo wa breki, hali iliyosababisha gari kurudi nyuma kwa kasi kabla ya kuteleza na kupinduka. Ameeleza kuwa miili imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same.

Mkuu huyo ametoa pole kwa familia za waliopoteza maisha na kuwaombea faraja katika kipindi hiki cha majonzi.

Katika tukio jingine, mtu mmoja amefariki dunia na wengine 52 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Moshi kuelekea Dar es Salaam kupata ajali katika eneo la Njoro, wilayani Same.

"Ajali hii imetokea saa saba usiku ikihusisha basi lililokuwa likitoka Moshi kuelekea Dar es Salaam. Watu 52 wamejeruhiwa na mmoja amepoteza maisha," amesema DC Mgeni.

Mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumzia majeruhi, DC mgeni amesema wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali za Same na Mwanga.