Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dereva anayedaiwa kusababisha kifo cha OCD Chico akamatwa Mbalizi

Muktasari:

  • Ajali ilitokea asubuhi ya Machi 17, 2025 eneo la Pugu Mwisho wa Lami jijini Dar es Salaam.na kumuua Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika (OCD), Awadh Chico na kumjeruhi kwa kuvunjika mkono askari, Zubeda Sadala

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemkamata dereva wa daladala anayedaiwa kusababisha ajali iliyomuua Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika (OCD), Awadh Chico, na kumjeruhi askari Zubeda Sadala.

Dereva huyo, Elia Asule Mbugi maarufu Dogo Bata (25), mkazi wa Segerea, jijini Dar es Salaam, alikuwa akiendesha gari aina ya Tata (daladala) na alitoroka baada ya ajali.

Ajali hiyo ilitokea Jumatatu, Machi 17, 2025 saa 1:20 asubuhi , katika Barabara ya Nyerere maeneo ya Pugu Mwisho wa Lami, jijini Dar es Salaam, ikihusisha gari aina ya Tata inayofanya safari zake kati ya Zingiziwa Chanika na Machinga Complex Ilala, ikitokea Pugu kwenda Gongo la Mboto. Gari hiyo iligongana na gari ndogo aina ya Toyota Prado.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Machi 30, 2025, Kamanda Muliro amesema, "Mtuhumiwa huyo alikamatwa na makachero wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam tarehe 27 Machi 2025 huko maeneo ya Mbalizi mkoani Mbeya. Atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo."