Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajali yaua wanakwaya Njombe

Muktasari:

  • Hata hivyo, habari ambazo hazijathibitishwa zinaeleza kuwa kuna idadi kubwa ya majeruhi kwenye ajali hiyo ambayo haijafahamika idadi kamili.

Njombe. Ajali iliyohusisha basi dogo aina ya Toyota Coaster na lori lililobeba makaa ya mawe, imekatisha maisha ya watu watatu wakiwemo waimbaji wa Kwaya ya Vijana wa Kanisa Katoliki mkoani Njombe (UVIKANJO).

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea usiku huu eneo la Igima wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe.

Taarifa zinaeleza kuwa wanakwaya hao walikuwa njiani kwenda kuwatembelea watoto yatima katika kituo cha Ibumila kilichopo wilayani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa kwa sasa wako eneo la tukio katika harakati za uokoaji.

“Ni kweli tukio hili limetokea kwa sasa tupo huku maporini bado tunaendelea na uokoaji, mvua ni kubwa na kazi ni ngumu taarifa kamili tutaitoa baadaye. Kuna majeruhi tumewawahisha hospitalini na vifo vipo,” amesema Issah.

Hata hivyo, habari ambazo hazijathibitishwa zinaeleza kuwa kuna idadi kubwa ya majeruhi kwenye ajali hiyo ambayo haijafahamika idadi kamili.

Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kupata mfululizo wa matukio kwenye ajali hiyo kupitia tovuti ya mwananchi na mitandao yake ya kijamii kama Instagram, Facebook na Twitter.