Wafuasi Chadema wakamatwa Kisutu, kesi ya Mbowe kwa kamera

Muktasari:
- Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuzuiwa kuingia ndani wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Dar es Saalaam. Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuzuiwa kuingia ndani wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Wafuasi hao waliokuwa wamefika kwaajili ya kufuatilia kesi ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye hata hivyo hakufikishwa mahakamani walikamatwa baada ya kutoa mabango yenye jumbe mbalimbali na kuanza kuimba.
Soma zaidi hapa: Ulinzi umeimarishwa Mahakama ya Kisutu
Askari waliokuwa kwenye magari mawili waliteremka kisha kuwazunguka na kuwakamata baadhi yao na wengine kufanikiwa kukimbia.
Mbowe ambaye alifikishwa mahakamani hapo, Julai 26, 2021 anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kula njama za kutenda kosa na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi, huku wenzake watatu wao wakikabiliwa na mashtaka saba.