Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MCL inavyoimarisha afya, usalama kwa wafanyakazi

Muktasari:

  • MCL ilipambana na majanga ya Uviko- 19 mwaka 2020, janga la moto mwaka 2023 na Homa ya nyani (Mpox) mwaka huu

Dar es Salaam. Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Afya na Usalama leo Jumatatu, Aprili 28, 2025, Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) imeeleza namna inavyotekeleza kwa vitendo usalama na afya kwa wafanyakazi wake mahala pa kazi.

MCL inayojishughulisha na uzalishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na MwanaSpoti, uandaaji wa Jukwaa la Fikra na usafirishaji wa mizigo imebainisha jinsi inavyopambana kuhakikisha wafanyakazi wake wanakuwa salama wakati wote.

Akizungumzia mikakati ya kampuni hiyo, Meneja Usalama wa MCL, Apolo Ogala amesema imekuwa mstari wa mbele kuhakisha usalama na afya mahali pa kazi.

Ametolea mfano namna kampuni ilivyopambana na majanga ikiwamo ya Uviko- 19 mwaka 2020, janga la moto mwaka 2023 na Homa ya nyani (Mpox) mwaka huu, akisema MCL iliweka mazingira rafiki kwa wafanyakazi kukabiliana na majanga hayo na walifanikiwa.

"Nikianzia nyuma wakati wa Uviko-19 ilisababisha kazi nyingi kusimama katika nchi mbalimbali duniani, ulipoingia nchini Tanzania kilikuwa ni kipindi kigumu kama kwa wenzetu wengine.

"MCL wakati ule ilikuja na mpango mkakati mzuri, kwa kufikia uamuzi wa wafanyakazi wake kufanyia kazi nyumbani bila kukutana ofisini, mkakati ambao ulisaidia sana," amesema Ogala.

Amesema walifanikisha programu hiyo kwa asilimia kubwa, ikiwamo wafanyakazi kupewa vitendea kazi ili kutekeleza majukumu yao wakiwa nyumbani.

"Lengo lilikuwa kupunguza mikusanyiko, kama kampuni tulifanikiwa, lilibaki kundi dogo la watu wachache ambao hawa ilikuwa ni lazima wafike ofisini kutokana na majukumu yao.

"Kwa wale wachache walioendelea kuja kazini walipewa barakoa na vitakasa mikono, tuliweka pia vitakasa mikono vingine kuanzia geti kuu na kuhakikisha tunachukua tahadhari zote," amesema Ogala.

Amesema wafanyakazi waliokuwa kazini walihakikisha pia wanafanya kazi kukiwa na 'distance' kutoka meza moja na nyingine na mara kadhaa walifanya check-up kujua afya zao.

"Tulikwenda kwa tahadhari hiyo kipindi chote na kuhakikisha tunawalinda wafanyakazi na wakati huo huo kazi zikiendelea,” amesema Ogala.


Moto kiwandani

Meneja huyo amesema kabla janga hilo halijapoa vizuri, mwaka 2023 kukatokea jingine la moto makao makuu ya MCL, Tabata jijini Dar es Salaam.

Akielezea janga hilo, Ogala amesema moto uliunguza stoo ya kampuni, kwa kuwa kampuni ilikuwa imejipanga, moto ule haukuleta madhara kwa binadamu.

"Alarm yetu iligundua na kutoa ishara ya hatari, watu walipambana nao kwa hatua tukitumia fire extinguisher kabla ya kufika magari ya zimamoto kwa uokozi zaidi," amesema.

Amesema mbali na changamoto hizo, mwaka huu pia japo haikuwa kwa kiasi kikubwa, ilipotangazwa kuwepo kwa watu waliogundulika kuwa na Homa ya Nyani (Mpox) MCL ilijipanga kuchukua tahadhari zote kwa wafanyakazi.

"Mpox ilitukuta tumeshafanya jithada na kujitayarisha kwa tahadhari zote, hivyo mpaka sasa hatujapata changamto ya mtu kuumwa, zaidi tulirudi kwenye utaratibu wetu wa kuchukua tahadhari tukiamini kinga ni bora kuliko tiba," amesema.

Amesema katika tahadhari hizo, mbali na kufanya mafunzo ya mara kwa mara na kubandika mabango ya kuelimisha wafanyakazi na wageni waliofika MCL, iliweka vitakasa mikono kwenye kila kitengo na kuhakikisha kila anayeingia kwenye ofisi hiyo ana takasa mikono.

Ogala amesema tahadhari zote zilichukuliwa kwa uzito na kuzingatiwa na kila mmoja ofisini hapo.

"Menejimenti ya MCL iliwezesha tahadhari hizi kufanyika kwa ufanisi, vilevile wafanyakazi wote walitoa ushirikiano mkubwa, hawakubaki nyuma kwa kuona kazi ya tahadhari ni ya idara fulani.

"Kila mfanyakazi aliguswa na alichukua tahadhari, kila mmoja alijitoa kusaidia kuhakikisha usalama na afya katika nyakati zile ngumu vinaimarishwa," amesema.

Amesema kampuni itaendelea kuchukua tahadhari zote kuhakikisha usalama na afya za wafanyakazi vinaimarishwa, akigusia pia kuhusu mkakati wa tahadhari ya moto.

Ogala amesema MCL kuna mfumo ambao linapotaka kutokea janga la moto unagundua mapema chanzo.

"King’ora kitalia na wafanyakazi wote watajua kuna hali ya hatari, watatoka nje kwenda assembly point ili kupata maelekezo zaidi ya usalama.

"Hadi sasa wafanyakazi wengi wanafahamu nini cha kufanya na wapo tayari kwa tahadhari, habari njema ni kwamba wengi wao wanafahamu kutumia fire extinguisher kwa uokozi wa awali inapokea janga la moto," amesema Ogala.


Walichokisema wafanyakazi

Mfanyakazi wa chumba cha habari, Ruth Liana amesema MCL imejizatiti katika kuchukua tahadhari zote za majanga.

"Nakumbuka wakati wa Uviko-19, ilikuwa ni lazima uwe na barakoa na utakase mikono ndipo uingie ofisini, hii ilitusaidia sana wafanyakazi tuliokuwa tunaingia kazini na majukumu yakaendelea kwa ufanisi," amesema Liana.

Mwandishi wa gazeti dada la Mwananchi, la The Citizen, Majuto Omary amesema tahadhari za MCL haziishi kwenye majanga pekee.

"Hata katika majukumu ya kazi ngumu ambazo zinakuwa na matukio ya Jeshi la Polisi, huwa wanatoa tahadhari na kutaka waandishi wake kuchukua tahadhari zote.

"Huwa tunapewa semina, ukiwa field (kwenye kazi) ukipata tatizo kuna namba za dharura utapiga ili upate msaada wa haraka,” amesema.

Nasra Abdallah, mwandishi wa habari wa Mwananchi amesema mara kwa mara MCL imekuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi juu ya afya na usalama kazini.

Amesema mafunzo hayo yamekuwa yakiwasaidia wafanyakazi wengi kuwa na uelewa wa tahadhari.