Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vitisho chanzo cha kutoripoti ukatili kijinsia

Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi Manispaa ya Morogoro wakifuatilia matukio wakati wa kilele cha siku ya familia duniani zilizofanyika kimkoa katika Shule ya Msingi Mwere. Picha na Juma Mtanda.

Muktasari:

  • Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Manispaa ya Morogoro wameelezea watu wanaotekeleza matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na ulawiti, hutumia mbinu ya vitisho kama njia ya kumzuia muathirika kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika.

Morogoro. Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Manispaa ya Morogoro wameelezea watu wanaotekeleza matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na ulawiti, hutumia mbinu ya vitisho kama njia ya kumzuia muathirika kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika.

 Kwa mujibu wa wanafunzi hao, vitisho humsababisha mtoto aliyekumbwa na tukio hilo kuogopa kulifichua akihofia usalama wake.

Wakizungumza leo Jumatatu Mei 15, 2023 mbele ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatuma Mwassa, katika kilele cha siku ya familia duniani, kwa nyakati tofauti, wanafunzi hao wamesema kuwa vitisho husababisha muathirika kushindwa kutoa taarifa.

Mfano, Mwanafunzi wa shule ya msingi Mchikichini B, Witness Pastory amesema waathirika wa ukatili wa kijinsia, umekuwa tatizo sugu kutoka na vitisho hivyo.

“Watoto waliopitia ukatili wa kijinsia kwa kubakwa, kulawitiwa na wengine kupata ujauzito, hushindwa kusema wakihofiwa kuuwawa na hasa hatua zile za awali za tukio likiwa bado bichi, na hii inatokana na vitisho wanavyopewa na wale wanaotekeleza ukatili huo,” amesema Witness.

Kwa upande wa mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari ya Morogoro, Mwanakobo Burhan Ally; ili kufichua siri za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike na kiume, wanapaswa kutokubali vitisho na watoe siri ya mtu aliyefanya tukio hilo kwa kueleza kwa mzazi, mlezi au mtu ambaye yupo karibu nao.

“Kwa wanafunzi wa kike waliopevuka hasa kuanzia darasa la sita na saba kwa shule za msingi, na wale wanaosoma shule za sekondari; waachane na tamaa na kukubaliana na hali ya maisha wanaoishi, kwani kinyume na hapo, hatari inawanyemelea ya kubakwa na kupata ujauzito ambao utakatisha ndoto za maisha yao.” amesema Mwanakobo.

Mwanakobo amesema tamaa kwa baadhi ya watoto wa kike, zimekuwa zikipelekea kukumbana na changamoto ya kuingia katika mahusiano yanayopelekea kutotimiza malengo yao.

Kwa upande wa Mkuu wa mkoa huo, amesema kipindi cha nyuma, wazazi wengi walikuwa na mifumo bora ambayo ilichangia malezi bora katika familia na kutengeneza kizazi bora na chenye heshima, tofauti na sasa ambapo kuna mmomonyoko wa maadili.

“Mwaka 2021 katika madawati ya jinsia na watoto ya kipolisi mkoani wa Morogoro, jumla ya matukio 347 yaliripoti, na kwa mwaka 2022; jumla ya matukio 303 yalilip[otiwa. Hata hivyo, kwa kipindi cha Januari hadi April 2023, vitendo vya ukatili vilivyoripotiwa ni 648,” amesema Mwasa.

Mkuu huyo wa mkoa ametanabaisha kuwa, kwa kipindi hicho peke, waathrika wenye umri wa mwezo 0 hadi miaka 18, kulikuwa na matukio 342. Wakati kwa wale wenye umri wa kati ya miaka 19 hadi 35 ni matukio 210.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, kwa wa miaka 36 hadi 70, jumala ya matukio 96 yaliripotiwa, na kwamba serikali imechukua hatua na kesi 620 zimefunguliwa na watuhumiwa 388 wamekamatwa na kwamba wapo katika hatua mbalimbali za kiuchunguzi.