Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UVCCM: Busara za viongozi zachochea amani, maendeleo Zanzibar

Muktasari:

  • Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Rehema Sombi, amepongeza busara za chama hicho kukubali kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa maslahi ya Wazanzibari, huku akikitabiria ushindi chama chake.

Zanzibar. Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Rehema Sombi, amepongeza busara za chama hicho kukubali kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa maslahi ya Wazanzibari, huku akikitabiria ushindi chama chake.

Makamu Mwenyekiti huyo wa UVCCM, ametoa pongezi hizo leo Jumamosi Septemba 9, 2023, katika mkutano uliofanyika Pemba, uliokuwa unahitimisha ziara ya kamati ya utekelezaji ya UVCCM, inayoongozwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Mohamed Ali Kawaida

“Busara za viongozi zimerejesha amani...sasa tunaijenga nchi yetu kwa pamoja, tunakosoana, tunarekebisha, lakini mwisho wa siku tunakubaliana kwenye ujenzi na mustakabari mwema wa nchi yetu,” amesema Sombi na kuongeza;

“Haya yote yanafanyika kwa sababu Serikali ya CCM inaongozwa kiungwana, na ndio maana ilikubaliana na uwepo Serikali ya Umoja wa Kitaifa, licha ya kuongoza kwa wingi kura lakini pia wingi viongozi katika vyombo vya uamuzi.”

Kwa mujibu wa Sombi, kabla ya Mapinduzi ya Januari mwaka 1964, wananchi walikua hawashirikishwi katika katika uamuzi kuhusu ustawi wa maendeleo.

Kwa upande mwingine Sombi amekitabilia chama cjake ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao akisema: “Kutokana na utekelezaji wa ilani ya chama, tuna uhakika Rais Samia Suluhu Hassan na Dk Hussein Mwinyi, wataibuka kidedea katika uchaguzi mkuu 2025.”

Amesema viongozi hao wawili wamejitahidi kuleta maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za afya Zanzibar na Tanzania bara na kwamba wana uhakika watashinda kwa hata kwenye majimbo ya majimbo ya Pemba, ambako kunaonekana kuwa ngome ya upinzani.

"Kuna watu wamezoea kusema CCM haikubariki Pemba watakuwa wanajidanganya kwa sababu kwa kasi ya utendaji kazi wa Rais Samia na Dk Mwinyi, lazima ushindi utakuwa kwa CCM pekee," amesema Sombi.