Ulinzi waimarishwa Kisutu, Lissu akifikishwa mahakamani

Dar es Salaam. Wakati, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu akiwa ameshafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusikiliza kesi zake mbili, ulinzi katika Mahakama hiyo umeimarishwa.
Ulinzi huo umeanzia katika lango la kuingilia katika Mahakama hiyo hadi katika ukumbi namba moja ambapo kesi hizo mbili zitasikilizwa hapo.
Lissu amefikishwa mahakamani hapo saa 2:45 asubuhi na kupelekwa mahabusu iliyopo katika Mahakama hiyo.
Leo Jumanne Julai Mosi, kesi zake mbili zitatajwa katika Mahakama hiyo kwa mahakimu wawili tofauti.
Endelea kufuatilia mitandao ya kijamii ya Mwananchi.