Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania kinara uchumi jumuishi ikifanya vizuri pesa mtandao

Mkurugenzi wa Sera za Umma wa Shirikisho la Kampuni za Simu GSMA, Caroline Mbugua

Muktasari:

  • Kutokana na utafiti uliofanywa na Shirika la kimataifa linalounganisha mfumo ikolojia wa simu ili kugundua, kuendeleza na kutoa ubunifu unaosaidia biashara na jamii kustawi (GSMA) umeonyesha kuwa Watanzania wengi hawajaunganishwa Pesa Mtandao (Mobile Money).

Dar es Salaam. Kutokana na utafiti uliofanywa na Shirika la kimataifa linalounganisha mfumo ikolojia wa simu ili kugundua, kuendeleza na kutoa ubunifu unaosaidia biashara na jamii kustawi (GSMA) umeonyesha kuwa Watanzania wengi nchini hawajaunganishwa Pesa Mtandao (Mobile Money).

Akiwasilisha yaliyomo kwenye utafiti huo Mkurugenzi wa Sera za Kijamii, Kusini mwa jangwa la Sahara, Caroline Mbugua amesema Tanzania imeonekana kuwa na ushuru mkubwa karibu mara mbili ya nchi zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwa na asilimia 47 kwenye Pesa Mtandao.

Hata hivyo Tanzania imefanya vizuri kwenye uchumi jumuishi ikifanya vizuri kwenye Pesa Mtandao.

Ni asilimilia 52 pekee ya Watanzania (watu wazima) wanaotumia pesa mtandao chini zaidi ikilinganishwa na Uganda  asilimia 66, Kenya  asilimia 79 na Afrika Kusini asilimia 85.

GSMA imependekeza kuondolewa kwa makato kwenye pesa mtandao ili kuchochea ukuaji wa uchumi.