Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanesco kuanza uzalishaji umeme ziwa Ngosi

Muktasari:

Kampuni tanzu ya kuzalisha umeme ya Tanesco ya uendelezaji joto nchini (TGDC) itaanza kuzalisha umeme Novemba 2022 kutoka kwenye chanzo kilichopo ziwa Ngosi lililopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Mbeya. Kampuni Uendelezaji Joto nchini (TGDC) imetenga zaidi ya Sh321.2 bilioni kwa ajili ya kuzalisha megawati 70 za umeme kutoka kwenye maji ya moto yanayopatikana ziwa Ngosi lililopo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Hayo yameelezwa jana Septemba 19, 2022 na Mwenyekiti wa Bodi ya uendelezaji joto ardhi nchini Tanzania TGDC ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la umeme (Tanesco), Shubi Kaijage baada ya kufika eneo ambapo mradi wa utazalishaji umeme unatarajia kujengwa.

Kaijage amesema umeme huo utakapoanza kuzalishwa utasaidia kupunguza changamoto ya umeme nchini ambapo ameeleza kuwa tayari maandalizi yote yamefanyika ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti katika eneo hilo la ziwa.

"TGDC imeshakamilisha utafiti wa kitaalam kwa ajili uendelezaji wa jotoardhi katika ziwa Ngosi, tumeagiza mitambo ya kucholonga visima vya kuzalisha umeme ambayo itawasili nchini mwezi ujao na hivyo kazi hiyo tutaoanza hapa Novembar mwaka huu," amesema Profesa Kaijage.

Amesema wamejipanga kuhakisha wanaisimamia vyema kampuni ya uendelezaji joto ardhi nchini ili kuhakikisha mipango iliyowekwa inatekelezeka kwa wakati na kwa ufanisi.

Kwa upande wa mjumbe wa bodi, Lucy Sondo akizungumza baada ya kuona chanzo hicho amepongeza juhudi zinazofanywa na TGDC kwa kufikia hatua ya kuzalisha umeme kutumia joto ardhi linalopatikana kwenye ziwa ngosi.

"Kutoka na uhifadhi wa msitu ulivyo kwenye eneo la ziwa naamini kuwa chanzo hicho kinakwenda kupunguza changamoto ya umeme baada ya kuanza uzalishaji, amesema Sondo," amesema.

Naye Abel Kabage ni mwananchi wa eneo hilo amesema kuanza kwa mradi huo kutachochea uchumi wa wakazi wanaozunguka eneo la ziwa na kuinua maendekeo ya wananchi.

Aidha Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya uendelezaji joto ardhi Shakiru Idris akizungimzia mradi huo amesema maandalizi yote ya kuanza ucholongaji wa visima vya maji moto kwa ajili ya kuzalisha umeme yamekamikika na ifikika mwezi Novemba watakuwa wameamnza uchorongaji.