Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Takukuru Mtwara yatoa maagizo watumishi Afya

Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mtwara, Enock Ngairo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) Florence Sanawa

Muktasari:

Watumishi wa afya wametakiwa kuacha kutumia mifumo ya utoaji wa dawa vifaatiba bila ya kuwa na  fomu maalumu iliyosainiwa na afisa anayeomba vifaa hivyo.

Mtwara. Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mtwara, Enock Ngairo amewaonya watumishi wa afya kuacha kutumia Mifumo ya utoaji wa dawa vifaatiba  bila kuwa na  fomu iliyosainiwa na ofisa anayeomba vifaa hivyo.

  

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo  alisema kuwa kwenye uchambuzi wa mfumo wa utoaji dawa na kupokea dawa na vifaatiba umekuwa ukifanyika kwa ajili ya kwenda kutumia kwa wagonjwa.


Alisema kuwa baadhi ya dawa zinatolewa stoo hazionekani katika rejista ya kutolea kwa wagonjwa hali ambayo inazua maswali.

 “Upo upotevu wa dawa tumegundua hilo na kazi yetu kubwa ni kuchunguza ndio maana tumefungua majalada ya uchunguzi bado thamani haijafahamika. Tunashirikiana na watalaamu wengine kufanya uchugnuzi ili baadaye tuje na majibu kuwa hasara ni kiasi gani lakini uchunguzi unaendelea kwasababu halmashauri zote zina tatizo hilo,” amesema Ngairo.


Katika hatua nyingine kamanda huyo alisema kuwa eneo la uzuiaji rushwa, mkoa umejipanga kufuatilia utekelezaji wa miradi ishirini na moja yenye thamani ya zaidi ya Sh10 bilioni katika sekta ya ujenzi, elimu, afya na maji.


 “Ipo miradi mitatu sawa na asilimia 14 ilikuwa na mapungufu madogo kama kuchelewa kukamilika kwa mujibu wa mkataba jambo linalosababisha kuongezeka kwa gharama,” amesema.


“Matumizi ya vifaa visivyokidhi ubora pamoja na manunuzi  kwa gharama zaidiya bei ya soko na kutofanyika kwa baadhi ya kazi zilizowekwa kwenye BOQ pia tumefanya chambuzi nne za mifumo katika sekta ya ilimo ushirika ujenzi na afya,” amesema.


“Tumebaini kwamba kwenye uchambuzi wa mfumo wa manunuzi kwa kutumia njia ya ‘force account’ katika miradi ya afya kuna ufahamu mdogo kwa kamati za hospitali kuhusu mfumo huu katika manunuzi,” amefafanua Ngairo.