Hotuba ya kwanza ya Papa Leo wa XIV

Vatican City. Papa Leo wa XIV ametoa hotuba yake ya kwanza akiwa Papa kwa kutumia lugha ya Kiitaliano na Kihispania.
Baada ya maneno yake ya kwanza, “amani iwe nanyi nyote,” aliendelea na ujumbe wa mshikamano na maelewano.
“Ndugu na dada wapendwa, huu ndio mwamko wa kwanza wa Kristo aliyefufuka.
“Ningependa kutoa salamu za amani ziwafikie familia zenu, nyote, popote mlipo. Amani iwe nanyi.”
Aliongeza kuwa, “Mungu anatupenda sote bila masharti,” na akatoa heshima kwa mtangulizi wake, Papa Francis.
Aliwashukuru makardinali waliomchagua kama kiongozi wao mpya.
Mwishoni mwa hotuba yake, alihamia katika lugha ya Kihispania, akiwashukuru waumini wa jimbo lake la zamani nchini Peru, akisema watu waaminifu walishiriki imani yao na kutoa mengi.”
Alikumbuka miaka mingi aliyotumia kama mmisionari na baadaye askofu mkuu wa Chiclayo.
Licha ya kuzaliwa Chicago nchini Marekani lakini alihudumu kwa miaka mingi kama mmisionari nchini Peru kabla ya kuteuliwa kuwa askofu mkuu huko.
Miaka miwili iliyopita, Papa Francis alimteua kuchukua nafasi ya Marc Ouellet kama mkuu wa Idara ya Maaskofu ya Vatican, na hivyo kumpa jukumu la kuchagua kizazi kijacho cha maaskofu.
Wakati huohuo, Rais Donald Trump wa Marekani alitoa maoni yake kuhusu uteuzi huo, akituma salamu zake za pongezi kwa Papa Leo wa XIV kupitia Truth Social, na kuongeza:
“Ni heshima kubwa kutambua kuwa yeye ndiye Papa wa kwanza kutoka Marekani. Ni jambo la kusisimua sana, na ni heshima kuu kwa Taifa letu. Natarajia kwa hamu kukutana na Papa Leo wa XIV. Itakuwa wakati wa maana sana”.