Takukuru Kinondoni yaandaa kesi nne za rushwa

Muktasari:
Katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba 2022, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kinondoni imepokea taarifa ya matukio 45 za vitendo vya vitendo vya rushwa.
Dar es Salaam. Katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba 2022, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kinondoni imepokea taarifa ya matukio 45 za vitendo vya vitendo vya rushwa.
Hayo yameelezwa leo Desemba 2, 2022 na Kaimu Mkuu wa Takukuru katika mkoa huo, Ismail Suleiman jijini hapa alipozungumza na Mwananchi.
Suleiman amesema hadi sasa majalada manne ya uchunguzi yamekamilika na kupelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Amesema katika kipindi hicho kesi mpya tatu zimefunguliwa katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.
“Hivyo inafanya jumla ya kesi zinazoendelea mahakamani kuwa 23 na tayari kesi moja ilishatolewa hukumu na upande wa Jamuhuri kushinda kesi,” anasema.
Pia amesema wamefanya ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi minne yenye thamani ya bilioni 1.12 na kugundua upungufu ukiwemo utekelezaji wa mradi bila ya kuwepo na mkataba, malipo ya vifaa kufanyika kabla ya vifaa husika kusambazwa.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuepuka matapeli wanaoibuka na kuwapigia simu na kujifanya ni maafisa wa Takukuru na kuwatapeli kwa kuwatisha kuwa wana taarifa zao na kuwadai fedha ili wawasaidie kuzifuta tuhuma hizo.
Pia aliwataka kuendelea kutoa ushirikiano kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo na kuwasihi kuendelea kutoa taarifa pale wanapoona vitendo vyovyote vya rushwa