Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TMA yatangaza hali ya upepo mkali kwa siku mbili

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa TMA maeneo yatakayokumbwa na upepo mkali ni mikoa ya Pwani ikiwamo Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, pamoja na visiwa vya Pemba, Unguja na Mafia.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza hali ya upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa Pwani ya Bahari ya Hindi.

Maeneo yatakayokumbwa na upepo kwa mujibu wa TMA ni mikoa ya Pwani ikiwamo Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, pamoja na visiwa vya Pemba, Unguja na Mafia.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano, Mei 14, 2025 kwa vyombo vya habari imeeleza uwezekano wa upepo huo kutokea ni kuanzia kesho Alhamisi Mei 15 na kiwango cha wastani wa athari zinazoweza kutokea.

“Athari zinazoweza kujitokeza ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza Mei 16, kuna uwezekano wa kujitokeza hali kama hiyo katika mikoa ya Pwani ukiwamo Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, pamoja na visiwa vya Pemba, Unguja na Mafia na athari zinazoweza kujitokeza ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.

Februari 25, 2025, TMA ilitoa angalizo la uwepo wa upepo mkali na mawimbi makubwa, katika Pwani ya Kaskazini mwa Bahari ya Hindi.

Katika taarifa hiyo, iliitaja mikoa itakayokumbana na hali kuwa Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba, ikieleza kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani.