Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spika Ndugai aomba radhi Wakristo, Watanzania

Muktasari:

  • Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ameomba radhi waumini dini ya kikristo na Watanzania wote waliokwazika na kauli yake aliyoitoa leo asubuhi akieleza mstari wa Biblia.

Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ameomba radhi waumini dini ya kikristo na Watanzania wote waliokwazika na kauli yake aliyoitoa leo asubuhi akieleza mstari wa Biblia.


Akizungumza bungeni leo Agosti 31, Spika Ndugai amesema ameshatembelea Uyahudi na kwamba anajua maeneo aliyozaliwa Yesu.

“Uyahudi nimekwenda mara nne, nimefika Kapernaumu kule kwenye kijiji cha Yesu, Galilaya yote ile nimetembea naijua, Kana naijua.


“Nimefika Nazareth, najua unaposema Yesu alitembea na mke wake kutoka Nazareth kwenda mpaka Yerusalem kuhesabiwa na wakakosa mahali pa kulala kutoka Yerusalem kwenda mpaka Betlehem alipozaliwa Yesu, distances zote zile nazijua.”


Hata hivyo, katika taarifa iliyotolewa leo Agosti 31, 2021 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, ofisi ya Bunge imefafanua kuwa, Spika Ndugai alimaanisha; “Yusufu alitembea na mke wake kutoka Nazareti kwenda Yerusalem kuhesabiwa na siyo Yesu kama alivyotamka awali.

“Hivyo, kilichotokea ni hali ya kibinaadamu ya ulimikuteleza ambayo huweza kumtokea mtu yeyote yule,” imefafanua taarifa hiyo.