Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh615 bilioni kujenga meli mpya, kiwanda cha meli

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli( MSCL), Eric Hamis (kulia) na mwakilishi wa mkandarasi kutoka kampuni ya M/S  Dearsan Gemi Insaat Sanayi As ya nchini Uturuki wakionyesha nakala ya moja ya mikataba waliyosaini ya ujenzi wa meli mpya na kiwanda cha kujenga meli mkoani Kigoma. Picha na Happiness Tesha

Muktasari:

Meli mpya ya mizigo itakayotoa huduma Ziwa Victoria ikiwa na uwezo wa kubeba tani 3,000 ya mizigo itajengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh133.4 bilioni na utakamilika ndani ya miezi 24 ya utekelezaji.

Kigoma. Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imesaini mikataba mitatu ya ujenzi wa meli mpya mbili na kiwanda cha kujenga Meli mkoani Kigoma.

Mikataba hiyo imesainiwa kati ya Serikali na kampuni ya M/S Dearsan Gemi Insaat Sanayi As ya Uturuki wakati wa hafla iliyofanyika mjini Kigoma leo Oktoba 11, 2023 na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.

Kupitia mikataba hiyo, Serikali itajenga meli mbili mpya za mizigo zitakazotoa huduma Ziwa Tangayika na Ziwa Victoria.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Eric Hamis amesema mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Meli utagharimu zaidi ya Sh322.7 bilioni na utakamilika ndani ya miezi 24 ijayo.

Amesema mradi wa ujenzi wa meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,500 ya mizigo itakayotoa huduma Ziwa Tanzganyika utagharimu zaidi ya Sh159.30 bilioni na utekelezaji wake utakamilika ndani ya kipindi cha miezi 36.

‘’Meli hiyo itakuwa na uwezo wa kupakia malori marefu 25 au mabehewa 25 ya reli ya kisasa na magari madogo 65 itatumia muda wa saa sita kusafiri kutoka Bandari ya Kigoma hadi Bandari ya Kalemie nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),’’ amesema Hamis

Meli mpya ya mizigo itakayotoa huduma Ziwa Victoria ikiwa na uwezo wa kubeba tani 3,000 ya mizigo itajengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh133.4 bilioni na utakamilika ndani ya miezi 24 ya utekelezaji.

Akizungumzia miradi hiyo, Waziri Mbarawa amesema utekelezaji wake unalenga kukuza biashara ndani na nje ya nchi kutokana na nafasi ya Tanzania Kijiografia katika Ukanda wa Maziwa Makuu.

“Kukamilika kwa miradi hii kutafungua fursa za kiuchumi, biashara na ajira kwa vijana,’’ amesema Profesa Mbarawa

Kuhusu kiwanda cha kujenga meli ambacho ni cha kipekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Profesa Mbarawa amesema kukamilika kwa mradi huo siyo tu kutawezesha Taifa kujitegemea katika shughuli za ujenzi wa meli, bali pia kutaokoa mamilioni ya fedha zainatumika sasa kujenga meli nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Huduma za Biashara ya Meli kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac), Nelson Cosmas amesema shirikia hilo la umma linashirikiana na taasisi zingine za Serikali kuhakiki michoro na kuipitisha.

‘’Tasac kwa kushirikiana na taasisi nyingine tuna jukumu la kusimamia hatua zote za ujenzi wa meli mpya na baadaye kusimamia uendeshwaji wake kwa mujibu wa sheria na kanuni za usafirishaji majini,’’ amesema Cosmas