Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yamwaga ajira mpya, omba hapa

Dar es Salaam. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara, Idara, Mashirika, na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs), imetangaza nafasi 2,224 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, ujuzi na moyo wa kizalendo kujiunga na utumishi wa umma katika nyanja mbalimbali.

Tangazo hili la ajira limetolewa Juni 5, 2025, likiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuongeza ufanisi ndani ya taasisi zake.

Nafasi hizi, ambazo ni za mkataba wa muda wote, zimegusa kada mbalimbali kuanzia uendeshaji, elimu, hadi teknolojia ya kisasa na zinatoa fursa ya kipekee kwa wataalamu waliohitimu na wenye motisha kutoa mchango wao katika maendeleo ya taifa.

Kwa mujibu wa tangazo hilo lililotolewa kupitia tovuti rasmi ya Ajira Portal (https://portal.ajira.go.tz/), nafasi zilizotangazwa ni pamoja na:

    • Afisa Kumbukumbu Daraja la II – nafasi 10

    • Dereva Daraja la II – nafasi 500

    • Mwalimu Daraja la III C (Fizikia) – nafasi 120

    • Mwalimu Daraja la III C (Biashara) – nafasi 700

(Tangazo jipya)

    • Mwalimu Daraja la III B (Uzalishaji wa Chakula) – nafasi 9 (Tangazo jipya)

    • Mwalimu Daraja la III C (Nishati ya Jua) – nafasi 11 (Tangazo jipya)

    • Mwalimu Daraja la III B (Huduma za Chakula, Vinywaji na Mauzo) – nafasi 22 (Tangazo jipya)

    • Mwalimu Daraja la III B (Ushonaji na Teknolojia ya Nguo) – nafasi 2 (Tangazo jipya)

    • Mwalimu Daraja la III C (Uchumi) – nafasi 850

Tangazo hilo limetolewa katika wakati muafaka ambapo Watanzania wengi, hasa vijana waliohitimu vyuo vikuu na taasisi za mafunzo ya ufundi, wanatafuta ajira na nafasi ya kutumia ujuzi wao kujenga taifa. Aidha, nafasi hizi zimegawanyika kwa kuzingatia uhitaji halisi katika maeneo ya elimu ya ufundi, teknolojia mbadala, pamoja na huduma zinazolenga ustawi wa jamii.

Wito umetolewa kwa wote wenye sifa kutuma maombi yao mapema kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14 Juni 2025, na waombaji wanashauriwa kuepuka kusubiri dakika za mwisho ili wasikose fursa hii muhimu.

Mchakato wa kuomba ni rahisi, ambapo mwombaji anapaswa kujiandikisha kwenye tovuti hiyo, kuchagua nafasi anayohitaji, na kuambatisha nyaraka muhimu kama vyeti vya taaluma, cheti cha kuzaliwa, pamoja na wasifu binafsi (CV).

Serikali imesisitiza kuwa waombaji wote wanatakiwa kuwa waadilifu, wenye uzalendo, na waliojitoa kwa dhati kuhudumia taifa katika maeneo watakayopangiwa kufanya kazi.