Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali mbioni kutangaza ajira 45,000

Dodoma. Serikali imesema kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha itakuwa imetangaza nafasi za ajira mpya 45,000 kwa kada mbalimbali ambazo utekelezaji wake unafanyika.

Mwaka wa fedha wa Serikali unakwisha Juni 30 ya kila mwaka, hivyo kwa kauli hiyo, kuna nafasi za ajira zitakazotolewa ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Jumanne Mei 27, 2025 na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu ambaye amesema katika mwaka wa fedha 2025/26 Serikali imeidhinisha  jumla ya nafasi 41,500 za ajira mpya kwa kada mbalimbali ambazo zitawalenga kuajiri wahitimu stahiki.

Naibu waziri alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga ambaye ametaka kujua Serikali ina mpango gani wa kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo nchini.

Sangu amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imetoa nafasi 47,404 za ajira mpya kwa kada mbalimbali ambazo utekelezaji wake unaendelea kupitia sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma na mamlaka nyingine na wasailiwa kutoka vyuo mbalimbali waliofaulu  wamepangiwa vituo vya kazi.

“Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali inatarajia kutoa ajira mpya 45,000 kwa kada mbalimbali ambazo utekelezaji wake utafanyika kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha,” amesema naibu waziri.