Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaeleza ugumu kuwapata Watanzania waishio Sudan

Salmin Banga akizungumza kwa  niaba ya wanafunzi wenzake waliokuwa wanasoma Sudan mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax

Muktasari:

  • Watanzania 206 wamewasili nchini Salama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  kutoka Sudan huku Serikali ikieleza ugumu katika kuwapata Watanzania wanaoishi nchini humo

Dar es Salaam. Watanzania 206 wamewasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kutokea Sudan huku Serikali ikisema bado inaendelea na jitihada za kuwatafuta wengine waliobakia kuwarudisha nchini.

Watanzania hao ambao wengi ni wanafunzi waliokuwa wanasoma nchini humo wamerudi kufuatia mapigano yanayoendelea katika nchi hiyo baina ya kikosi cha Jeshi la Sudan (SAF) na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).

Akizungumza Dar es Salaam na vyombo vya habari leo Alhamisi,  Aprili 27,2023 katika hafla ya mapokezi hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax amesema kazi kubwa imefanyika hadi kuwapata Watanzania hao.

"Changamoto iliyopo Watanzania wengi hawajajisajili kwenye ubalozi wetu, ndiyo maana mnaona siku ya kwanza nilisema raia walioko tayari 200 lakini leo idadi imeongezeka, kuwapata imekuwa shida," amesema Dk Stergomena

Dk Stergomena ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa Watanzania wote wanaoishi mataifa ya nje kujisajili kwenye ubalozi ili changamoto zinapojitokeza iwe rahisi kuwasaidia.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Sudan, Salima Kombo Haji amesema ni  Watanzania wanne anaowafahamu wamebaki nchini Sudan.

"Kuna mmoja  alipoteza hati ya kusafiria dakika za mwisho, mwingine mtaalamu wa ngozi anafanya kazi kwenye kiwanda cha ngozi lakini dakika za mwisho alishindwa kutoka kwa sababu eneo hilo mapigano yalikuwa makubwa,”amesema

Amesema Wengine wawili wanafanya kazi kwenye migodi ya uchimbaji madini lakini wako maeneo mengine ambako machafuko hayako sana.

Kwa upande wake Salmin Banga aliyekuwa masomoni nchini Sudan Kwa niaba ya wanafunzi wenzake ameishukuru Serikali kwa kuonesha kuwajali kwani walikuwa kwenye wakati mgumu huku akieleza kuwepo kwa shida ya mawasiliano ya simu.