Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Machafuko Sudani yaathiri biashara ya mkonge nchini

Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), George Seni (aliyesimama) akifanya utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli (wa pili kulia), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TSB, SAddy Kambona ma kushoto ni Meneja Rasilimali Watu, Samson Ngatunga. Katibu Mkuu huyo amefanya ziara ya siku moja ambapo amekagua majengo ya Bodi na kuzungumza na watumishi.

Muktasari:

  • Kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Sudan, Tanzania ni miongoni mwa wahanga wa machafuko hayo kiuchumi baada ya kushindwa kupeleka oda ya magunia ya mkonge milioni 200 ambayo Sudan iliyaagiza Machi.

Tanga. Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona amesema mapigano yanayoendelea nchini Sudan yameathiri soko jipya la magunia milioni 200 ambalo walilipata nchini humo.

Kambona ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 25, 2023 jijini hapa wa wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya Sekta ya Mkonge kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli ambaye yupo mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi.

Amesema soko hilo jipya la magunia ya mkonge lilipatikana Machi baada ya ujumbe wa maafisa kutokana TSB kutembelea nchini Qatar kwa ziara ya kutangaza bidhaa zitokanazo na zao hilo.

"Miongoni mwa mafanikio ya ziara yetu nchini Qatar ni kupatikana kwa masoko ya bidhaa zitokanazo na mkonge nchi mbalimbali, ambapo Sudan pekee ilitoa oda ya magunia milioni 200 lakini vita inayoendelea imeathiri kwa kiasi kikubwa soko hilo kwa sababu hakuna kinachoendelea tena," amesema Kambona.

Mkurugenzi hiyo amesema hivi sasa magunia milioni moja yapo ghalani yakiwa tayari kusafirishwa kupelekwa Sudan lakini kutokana na machafuko hayo hiyo yamelazimu kihifadhiwa.

Nchi ya Sudan kwa sasa inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya wanajeshi wa Serikali na kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF) wanaogombania kushika hatamu ya kuiongoza nchi hiyo.

Akizungumzia kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya mkonge tangu mwaka 2020 baada ya Serikali kufanya maboresho ya bodi hiyo, Kambona amesema uzalishaji wa zao hilo umeongezeka kutoka tani 36,000 hadi tani 48,000 ilipofika Desemba 31, 2022 

Wakati eneo linalolimwa zao hilo la kimkakati likiongezeka kutoka hekta 46,000 mwaka 2018 hadi hekta 67,000 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 45.6

"Changamoto iliyopo kwa sasa ni mashine ndogo za kuuchakata zinapunguza ubora wa nyuzi na pia korona zilizopo hazitoshelezi mahitaji, bodi na wadau wengine tupo katika mikakati ya kujinasua kwenye changamoto hii," amesema Kambona.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema Serikali inalitegemea kwa kiasi kikubwa zao la mkonge na ndiyo maana iliamua kufanya maboresho kuanzia kukarabati jengo la ofisi ya TSB kwa Sh500 milioni na kuongeza watumishi kutoka 16 waliokuwepo mwaka 2020 hadi kufikia 37 waliopo sasa.